WAZIRI KAIRUKI ATEMBELEA OFISI ZA DART

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi ) Mhe.Angela Kairuki akisalimiana na watumishi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za DART leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam.

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi ) Mhe.Angela Kairuki amewapongeza Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) kwa kuweka mifumo imara ya ukusanyaji mapato na kutaka kuendelea kufanya tathimini ya ukaguzi wa kila mara.

Ametoa pongezi hizo leo Oktoba 10,2022 wakati alipofanya ziara ya kutembelea ofisi za za DART ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Amesema DART inapaswa kuhakikisha kunakuwa na huduma ya usafiri ambayo inahimilika kwa wananchi wenye vipato vya aina zote.

" Sisemi bei zifutwe, sisemi pia bei ziwe kiasi gani, lakini wataalamu warudi waangalia kwa jicho la kibiashara lakini wakati huo huo jicho la wananchi."amesema Waziri Kairuki

Aidha ameipongeza DART Kwa kuja na mpango wa kuongeza mabasi 177 yanayotumia gesi asilia sambamba na kupongeza hatua ya kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 37.16 baada ya kukusanya Sh bilioni 10.8 katika robo ya kwanza ya mwaka.

Aidha, Waziri Kairuki ameagiza kuipitia mikataba ya ubia ya uendeshaji mabasi kwa kuangalia vifungu vinavyohitaji utekelezaji ili utekelezaji ufanyike kwa wakati.

Kuhusu ujenzi wa miundombinu, Waziri Kairuki amewataka kuhakikisha wanakuwa ndani ya wakati huku akipongeza utekelezaji wa awamu ya pili ambayo imefikia asilimia 66.

Waziri Kairuki amemshukuru Rais Samia kutoa Sh bilioni 7.8 kwa ajili ya karakana na kuutaka uongozi kuhakikisha inafuata sheria katika kufanya tathmini na kulipa fidia kwa wakati.

Aidha ameihimiza DART kuendelea kutumia mifumo na teknolojia katika utendaji kazi wa Wakala na utoaji huduma kwa kuangalia mifumo ambayo itatoa unafuu wa gharama kwa kiasi kikubwa

Kwa Upande wa Mtendaji Mkuu wa DART Dkt.Edwin Mhede amesema kuwa lengo ya DART ni kusafirisha abiria 450000 kutokana miradi ya ujenzi ya miundombinu itakapokamilika.

Dk.Mhede amesema kuwa mapato yanaongezeka kila mwaka kutokana na mipango na mikakati katika kupata fedha ambayo uaminifu wao kwa serikali

Amesema kuwa hakuna sababu kuwepo katika wakala huo kama uzalishaji unakuwa wa kusuasua. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi) Mhe.Angela Kairuki akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za DART leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa DART Dkt.Edwin Mhede akizungumza mara baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi ) Mhe.Angela Kairuki kutembelea ofisi za DART leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya watumishi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi ) Mhe.Angela Kairuki (hayupo pichani) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea ofisi za DART leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi ) Mhe.Angela Kairuki akiagana na Mtendaji Mkuu wa DART Dkt.Edwin Mhede mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea ofisi za DART leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post