Katikati ni Profesa Joyce Ndarichako akizungumza na vyombo vya habari Mara baada ya kukagua maandalizi ya kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja na wiki ya vijana.
Na Mbuke Shilagi Kagera.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi vijana ajira na ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Albert Chalamila kwa maandalizi mazuri ya kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja na wiki ya vijana ambayo Kitaifa inafanyika Mkoa wa Kagera Manispaa ya Bukoba.
Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 11 Oktoba 2022, uwanja wa Kaitaba katika kukagua maandalizi ya kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge na wiki ya vijana Waziri Ndalichako amesema kuwa maandalizi ni mazuri kama alivyo kagua na kumpongeza Mkuu wa Mkoa pamoja na watumishi wake kwa maandalizi hayo.
Amesema kuwa kesho tarehe 12 Oktoba 2022 kutakuwa na uzinduzi rasmi wa wiki ya vijana katika viwanja vya Gymkana yaliyo anza tarehe 08 Octoba 2022 ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kasim Majariwa.
Huku akiongeza kuwa tarehe 14 Oktoba 2022 sherehe zitaanzia katika Kanisa kuu la katholiki Manispaa ya Bukoba kwa ibada ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Kisha baada ya ibada mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan atakagua shughuli za vijana katika hitimisho la maadhimisho ya wiki ya vijana Kitaifa katika viwanja vya Gymkana.
Na kwamba baada ya hapo atakuwa uwanja wa Kaitaba katika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru hivyo wananchi wote waweze kujitokeza kwa wingi siku hiyo.