Bw.Chitalu Chilufya anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za uma kiasi cha dola za kimarekani milioni 17 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 3 za Kitanzania , ambazo zilikua ni za kusambaza vifaa vya afya wakati alipokua bosi wa wizara hiyo.
Taasisi ya kupambana na rushwa nchini Zambia imesema Waziri huyo wa zamani anashtakiwa akiwa na katibu mkuu wa zamani wa wizara hiyo Mulalelo Kakulubelwa pamoja na wakurugenzi wengine watatu wa afya.
Wote wamekana mashataka hayo na wameachiwa kwa dhamana. Wanakua ni miongoni mwa watu mashuhuri kutiwa nani siku ya jana kwa tuhuma kadhaa.
Mwanachama wa upinzani Kelvin Bwalya Fube yeye ametiwa ndani kwa makosa ya dawa za kulevya ikiwemo pia utakatishaji w afedha haramu.
Social Plugin