NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Yanga imeondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Al Hilal ya Sudan, mechi ambayo imepigwa kwenye dimba la Al Hilal nchini humo.
Yanga Sc katika mechi ya kwanza akiwa nyumbani aliweza kulazimishwa sare ya 1-1 bao lililofungwa na Fiston Mayele lakini tofauti na leo ambapo amepokea kichapo cha bao moja na bila kuweza kupata bao lolote kwenye mchezo huo.
Social Plugin