Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Uandishi wa Vitabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Ofisi ya Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Shinanga imetoa Mafunzo ya Uandishi wa Vitabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea uwezo katika shughuli zao.
Mafunzo ya siku tatu yamefunguliwa leo Ijumaa Novemba 18,2022 na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo yakikutanisha watendaji wa Vyama vya Msingi vya Pamba (AMCOS) 174 kutoka halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga.
Akifungua mafunzo hayo, Prof. Tumbo amesema yataongeza ufanisi katika utendaji kazi na kupunguza hati chafu kwenye AMCOS zinazotokana na kukosekana kwa taarifa.
“Kwenye Vyama vya Msingi vya Pamba uwekaji taarifa haupo sawa , uwekaji risiti haujakaa sawa, uwekaji taarifa za wakulima bado haupo vizuri hivyo tumieni mafunzo haya kupata ujuzi ili mkabadilishe namna ya utunzaji taarifa.Mnapewa hati chafu siyo kwamba mmekula pesa lakini kumbe taarifa tu hazipo sawa”,amesema Prof. Tumbo.
“Katika mkoa wa Shinyanga tunavyo vyama vya msingi vya pamba 174. Wakulima wanaoleta pamba ni wengi kuliko wanachama, utunzaji mzuri wa taarifa ndiyo utawafanya muaminike na kupata wanachama wengi zaidi. Lakini pia hatutasikia kuhusu Hati chafu mfano ukaguzi uliopita kati ya vyama vya msingi 237 vilivyokaguliwa, vyama 7 pekee ndiyo vilipata hati safi, 57 hati ya mashaka na 176 zina hati chafu”,ameongeza Prof. Tumbo.
Amesema bado hali hairidhishi kwenye AMCOS ndiyo maana serikali inachukua hatua mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo kwa watendaji wa AMCOS ili vyama viweze kutunza taarifa hivyo kuwataka kwenda kutumia ujuzi watakaopewa.
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Hilda Boniphace amesema mafunzo hayo yamegawanyika katika vituo vinne vya kufundishia (Kahama vituo viwili, Shinyanga vituo viwili) kwa lengo la kuwajengea uwezo watendaji wa Vyama vya Msingi vya Pamba katika shughuli zao za kila siku.
“Matarajio ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) baada ya mafunzo haya ni kuona maendeleo ya ushirika, kuwe na uandishi mzuri wa vitabu utakaoondoa ama kupunguza Hati Chafu ili mwisho wa siku idadi ya vyama vinavyopata hati safi iongezeke”,amesema Hilda.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) Kwiyolecha Nkilijiwa amewataka watendaji katika AMCOS kufanya kazi vizuri ili kuiheshimisha SHIRECU ambayo sasa inaendelea kupiga hatua katika kujiimarishakwa kuhakikisha kuna taarifa sahihi na hakuna mambo ya ajabu ajabu kama wizi wa mali za ushirika.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Uandishi wa Vitabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Novemba 18,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Uandishi wa Vitabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Novemba 18,2022.

Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Hilda Boniphace akizungumza kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Vitabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) Kwiyolecha Nkilijiwa akizungumza kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Vitabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga

Mshiriki wa mafunzo hayo, Dioniz Nyalama akizungumza kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Vitabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga
Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Vitabu kwa vitendo
Viongozi wakiwa kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Vitabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin