Watumishi sita wa Serikali, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wakiwamo mke na mume, wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada ya kupata ajali ya gari eneo la Pori wilayani humo.
Watumishi hao kati yao watano wanatoka Idara ya Afya na mmoja Idara ya Elimu, kwa pamoja wamepoteza maisha baada ya gari lao walilokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na gari lingine aina ya Prado.
Tukio hilo limetokea jioni ya jana Jumatatu Novemba 07, 2022 eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo wilayani Kiteto na kupelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga amesema ajali hiyo imehusisha gari la wagonjwa la Kituo cha Afya Sunya lililokuwa limepeleka mgonjwa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa ajili ya matibabu na wakati likirudi likiwa limebeba watumishi kurejea eneo la kazi Sunya liligongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Prado likitokea barabara ya Kilindi Tanga kwenda Kiteto.
Chanzo - Mwananchi
Social Plugin