Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Chief Charumbira akizungumza katika Mkutano wa Bunge la Afrika leo Midrand Afrika Kusini.
Na Kadama Malunde - Midrand Afrika Kusini
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Chief Charumbira ameipongeza nchi ya Kenya kwa kufanya uchaguzi Mkuu wa amani na utulivu bila vurugu za uchaguzi akibainisha kuwa hiyo ni sehemu ya mkakati wa Umoja wa Afrika (AU) kunyamazisha Bunduki Barani Afrika.
Chief Charumbira ametoa pongezi hizo leo Jumatano Novemba 2,2022 wakati akitoa hotuba yake kwenye Mjadala wa Viongozi wa Juu wa Bunge Kuhusu Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala katika Afrika 'Mabadiliko ya Serikali yasiyofuata katiba na mageuzi ya kisiasa katika Afrika' wakati wa Kikao cha Tatu cha Mkutano wa Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika (Pan African Parliament - PAP).
"Tunapenda kuona amani na usalama barani Afrika na kuhakikisha Silaha zinanyamazishwa (Silencing the Guns). Tunashukuru Kenya hakukuwa na vurugu kabisa yoyote wakati wa uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni. Tume huru za uchaguzi zinatakiwa kuwepo mfano Kenya wameonesha mfano mzuri. Amani na usalama ni muhimu ili kutoathiri vipaumbele vya Umoja wa Afrika, ambavyo ni pamoja na utulivu, ukuaji wa uchumi, utoaji wa huduma za umma, kupunguza umaskini na kupambana na rushwa",amesema Chief Charumbira.
Chief Charumbira amesema mjadala huo unalenga kutafakari, kujadiliana, kubadilishana mawazo na kutoa mapendekezo juu ya nafasi ya Bunge la Afrika katika kukabiliana na ongezeko la matukio ya mabadiliko ya Serikali yasiyofuata katiba na mageuzi ya kisiasa barani Afrika.
Tume Huru ya uchaguzi ya Kenya (IEBC) ilimtangaza William Ruto kuwa Rais wa Kenya kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 9,2022 nchini humo.
Ruto alitangazwa mshindi mnamo Agosti 15,2022 baada ya kumshinda kiongozi wa Upinzani wa muda mrefu Raila Odinga ambaye baadaye aliomba ushindi huo katika Mahakama ya Juu ambapo kesi hiyo ilitupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Chief Charumbira akizungumza katika Mkutano wa Bunge la Afrika leo Midrand Afrika Kusini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Chief Charumbira akizungumza katika Mkutano wa Bunge la Afrika leo Midrand Afrika Kusini.
Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mhe. Chief Fortune Charumbira akizungumza katika Mkutano wa Bunge la Afrika leo Novemba 2,2022
High level Parliamentary Dialogue on Democracy, Human Rights and Governance in Africa
👇👇
Social Plugin