KAMATI YA UCHUNGUZI YA BWAWA LA MATOPE MGODI WA MWADUI YAKABIDHI RIPOTI KWA RC MJEMA KWA UTEKELEZAJI ZAIDI



* Mwenyekiti wa kamati Dc Mkude amemuhakikishia Mkuu wa mkoa Kamati imefanya kazi yake kwa weledi na ufanisi mkubwa wa kubaini chanzo, madhara, na njia za kuchukua.

* Rc Mjema ameipongeza kamati nzima kwa utendaji wake mkubwa, wataalamu na wote waliuhusika  katika kuandaa ripoti hiyo.

Na Michael Utouh - Shinyanga

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema siku ya leo amepokea ripoti ya uchunguzi wa bwawa la matope lililovunja kuta na kuelekea katika makazi ya wananchi mnamo tarehe 07.11.2022 katika mgodi wa Williamson Diamond limited uliopo Mwadui katika wilaya ya Kishapu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti hiyo mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph  Mkude amesema anamshukuru Mkuu wa mkoa kwa kuwa alikuwa ni wa kwanza baada ya kuripotiwa kwa janga hilo lililotokea katika mgodi aliweza kufika na kwa haraka na kuunda tume itakayochunguza chanzo Cha hadi kubomoka kwa bwawa

amesema kuwa lengo la kamati hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kuchunguza chanzo Cha kubomoka kwa bwawa, kubaini madhara yaliyotokea,kubaini madhara ya maji tope, lakini pia lengo la kamati hiyo ni kutoa ushauri na mapendekezo ya Nini kifanyike, na kufahamu hatua zilizochukuliwa na serikali, Mgodi pamoja na kuangalia kama kuna madhara yaliyojitokeza baada ya kubomoka kwa bwawa hilo

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amesema anaishukuru kamati hiyo ya uchunguzi ambayo imefanya kazi yake kwa weledi mkubwa na ufanisi hadi siku ya leo wanapoikabidhi kwake baada ya kufanya kazi ya uchunguzi kwa muda wote wa siku 14 toka alipoikabidhi kamati hiyo jukumu la kufanya uchunguzi huo

amesema ripoti hiyo ataifikisha kwa Waziri husika wa madini Mhe. Doto Biteko  na kupelekwa Baraza la usalama la mazingira ( NEMC) ambao ndio watakaotoa maamuzi ya mwisho baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo

Aidha Mhe. Mjema ameongeza kwa kusema Kamati hiyo aliyoiunda iliunganisha wataalamu wote wanaohusika katika kutoa taarifa iliyokamili baada ya kubomoka kwa bwawa hilo na sivyo kama wengi walivyokuwa wakidhani kamati aliyoiunda ni ya ulinzi na usalama tu 
 
Ametaja waliohusika katika kuandaa ripoti hiyo kuwa ni pamoja na wataalamu kutoka NEMC, Wizara ya madini kupitia time ya madini, wataalamu kutoka Blonde la maji kati, wataalamu kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali, kamati ya usalama ya Mkoa pamoja na ofisi ya DED kishapu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post