Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza kwenye la KKKT Ebeneza lililopo Mtaa wa Mbulu Manispaa ya Kahama.
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba amefanikisha kupatikana kwa shilingi Milioni 52 kati ya shilingi Milioni 100 zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kanisa la KKKT Ebeneza lililopo Mtaa wa Mbulu Manispaa ya Kahama.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa Harambee iliyofanyika katika kanisa hilo, Mhe. Santiel Kirumba ambaye amechangia kiasi cha shilingi Milioni 10 ameshukuru waumini wa kanisa hilo kushiriki kikamilifu katika harambee hiyo kwa kuchangia zaidi ya shilingi Mil 52 kati ya shilingi Mil 100 zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo.
Mhe. Kirumba ameiomba jamii kujenga tabia ya kuchangia ujenzi wa Nyumba za Ibada kwa ajili ya kujiweka karibu na Mungu sambamba na kujikomaza kiimani kulingana na imani za dini zao badala ya kuendelea kuchangia vitu mbalimbali kama sherehe zisizokuwa na tija kwenye maisha yao
Katibu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Yoram amesema wakati umefika wa jamii kubadilika na kuona umuhimu wa kuchangia ujenzi wa nyumba zao za badala ya kuendekeza kuchangia sherehe na vitu mbalimbali visivyo na tija kwenye maisha yao ya dini zao pamoja na familia zao hapo baadae.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza kwenye la KKKT Ebeneza lililopo Mtaa wa Mbulu Manispaa ya Kahama
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba na Katibu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Yoram (kushoto) wakijiandaa kukata keki kwenye la KKKT Ebeneza lililopo Mtaa wa Mbulu Manispaa ya Kahama
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kulia) na Katibu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Yoram wakikata keki kwenye la KKKT Ebeneza lililopo Mtaa wa Mbulu Manispaa ya Kahama
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akimlisha keki Katibu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Yoram (kulia).
Katibu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Yoram akimlisha keki Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba
Social Plugin