Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mhe. Chief Fortune Charumbira akizungumza katika Mkutano wa Bunge la Afrika leo Novemba 2,2022 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
***
Kikao cha Tatu cha Mkutano wa Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika (Pan African Parliament - PAP) kinaendelea muda huu leo Jumatano Novemba 2,2022 ambapo kuna Mjadala wa Viongozi wa Juu wa Bunge Kuhusu Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala katika Afrika 'Mabadiliko ya Serikali yasiyofuata katiba na mageuzi ya kisiasa katika Afrika'.
Katika Hotuba yake Rais wa Bunge la Afrika Mhe. Chief Fortune Charumbira amesema mjadala huo unalenga kutafakari, kujadiliana, kubadilishana mawazo na kutoa mapendekezo juu ya nafasi ya Bunge la Afrika katika kukabiliana na ongezeko la matukio ya mabadiliko ya Serikali yasiyofuata katiba na mageuzi ya kisiasa barani Afrika.
High level Parliamentary Dialogue on Democracy, Human Rights and Governance in Africa
👇👇
Social Plugin