Diwani wa kata Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani Mh. Nassar Karama
Diwani wa kata Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani Mh. Nassar Karama
NA ELISANTE KINDULU, CHALINZE
DIWANI wa kata ya Bwilingu katika Halmashauri ya Chalinze, Mh. Nassar Karama ameahidi huduma ya maji na umeme kwa wananchi na shule za msingi na Sekondari katika kata ya Bwilingu mkoa wa Pwani.
Mh. Nassar ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wakazi wa Kitongoji Cha Mdaula katika sherehe za mahafali ya darasa la saba yaliyofanyika tarehe Novemba 1,2022 katika viwanja vya shule ya msingi Mdaula.
Mh. Nassar alitanabaisha kuwa shule tatu katika kata yake tayari zinapata huduma ya maji ambapo pamoja na msaada wa wadau wengine wa maendeleo lakini pia zikiwemo jitihada za Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Ridhiwani Kikwete.
Aidha Mh. Diwani aliendea kusisitiza kuwa, Kata ya Bwilingu hakutakuwa na chaguo la pili na hivyo kufanya wanafunzi wote kuingia kidato cha Kwanza mwakani kutokana serikali kutoa shilingi milioni 600 katika shule mpya ya Sekondari Msolwa, shilingi milioni 60 za madarasa 3 katika Sekondari ya Mdaula, shilingi milioni 100 za madarasa 5 shule ya msingi Chahua na shilingi milioni 500 katika shule ya Sekondari ya Chalinze.
Wakati huo huo Mh. Nassar katika ziara yake katika Kitongoji cha Maluwi aliwaahidi wananchi wa Kitongoji hicho na maeneo mengine yatafikiwa na huduma ya umeme katika bajeti ya 2023/2024.
Social Plugin