Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ALIYEOLEWA NA MME WA RAFIKI YAKE NAYE APIGWA CHINI


Pete za ndoa

Mwanamke mmoja nchini Nigeria aliyemchukua mume wa rafiki yake na kuolewa yeye ameachwa na mwanaume huyo mara baada ya kujifungua.


Kupitia ukurasa wa Twitter wa Ufuoma umeeleza kwamba mwanamke huyo huyo baada ya kuachwa kwa talaka mara baada ya kujifungua amezindua kitabu kinachoelezea masaibu aliyokutana nayo ndani ya ndoa na mwanaume huyo huku yeye akijiona mwanamke wa shoka.

"Huyu mwanamke aliolewa na mume wa rafiki yake na baadaye mwanaume huyo alimtelekeza baada tu ya kujifungua na kumpa talaka na sasa anazindua kitabu cha maisha yake kuonesha kwamba ni mwanamke shupavu," amesimulia Ufuoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com