Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MANZI WA KIBERA AZUA GUMZO KUCHUMBIANA NA BABU WA MIAKA 65


Sosholaiti wa humu nchini Kenya anayetambulika kama Manzi Wa Kibera, amekaanga bila huruma kwenye mitandao ya kijamii, kwa kusaka kiki na mzee ambaye ametosha kuwa rika la baba yake.


Sosholaiti huyo amekuwa akisambaza picha na video zake akiwa na mzee huyo.


Kwenye mahojiano na Empire Group Production's YouTube channel, Mazni wa Kibera alidai kwamba yeye ni mpenzi wa mzee huyo wa miaka 65. Mrembo huyo alifafanua kwamba alimpenda mzee huyo kwa sababu humpa hela na kununua chohcote anachotaka.



Mzee huyo naye pia alikiri kwamba anachumbiana na Manzi wa Kibera. Katika ukurasa wa Nairobi Gossip, video ilisambazwa ikionyesha jinsi wapenzi hao walivyokuwa wakijivinjari katika hoteli moja.

Ila bado, wanamitandao hawakuamini, na kusama kwamba Manzi wa Kibera alikuwa akiyafanya mambo hayo ili kusaka kiki na mzee huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com