Kaimu mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la pangani Abrahamu Yesaya akiongea na wananchi wakati wa ufungaji wa mashindano ya ligi ya mpira ijulikanayo kwa jina la Nduruma cup iliyoandaliwa na bodi hiyo ya bonde la Pangani Kwa ajili ya kuhamasisha urejeshaji ,utunzaji wa mto Nduruma uliopo ndani ya wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
Mkurugenzi wa timu ya Charity Fc Izack Mgea akiongea na waandishi wa habari mara baada ya timu yake kuanda timu ya msitu wa mbongo Kwa penati tano Kwa tatu ambapo mchezo uliofanyika juzi na timu hii ikafanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi laki tatu kombe pamoja na mpira
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Luyangu akisalimiana na timu ya mpira wa miguu ya charity Tanzania Fc wakati wa fainali za mashindano ya Nduruma cup yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi wilayani Arumeru mkoani Arusha mashindano haya yaliandaliwa na bodi ya maji bonde la pangani Kwa ajili ya kuhamasisha urejeshaji ,utunzaji wa mto Nduruma uliopo ndani ya wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
watanzania wametakiwa kutunza na kulinda vyanzo vya maji kwani rasilimali hiyo ni adhimu ambayo haina mbadala, na inapaswa kutunzwa na kuendelezwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru muhandisi Richard Luyangu akiongea wakati akifunga mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo Kwa jina Nduruma cup yaliyoandaliwa na bodi ya maji bonde la pangani Kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja na kuurejesha wa mto Nduruma uliopo ndani ya wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Kwa kuchimba korongo la mto huo na kuelekeza maji kupita katika mkondo wake
Alisema kuwa ni vyema jamii ikajifunza kuishi maisha endelevu pamoja na kuzitunza rasilimali zinazotuzunguka haswa za maji kwakuwa maji ni uhai ,huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kuijenga mbali na vyanzo vya maji ikiwemo na kufuata sheria za utunzaji wa vyanzo hivyo
"Vyanzo vingi vya maji huku Arumeru vimekauka kutokana na wananchi kufunya shughuli za kibinadamu katika vyanzo hivyo ikiwemo kufanya kilimo katika vyanzo hivyo ,kukata miti hovyo bila kupanda pamoja na kuijenga katika vyanzo hivyo vya maji kitu ambacho ni hatari na kinapelekea maji kukauka"alisema
Aidha alibainisha kuwa serikali haitamfumbia macho mtu yeyote ambaye ataharibu Kwa njia yoyote Ile vyanzo vya maji ikiwemo kimchukulia sheria kali ikiwemo kumlipisha faini pamoja na kuwafikisha mahakamani
Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariti Daniel Palanjo alimshukuru waziri wa maji Juma Uweso Kwa kuagiza ligi hii ya mpira kuanzishwa kwani imetumika kusaidia kuwaeleza wananchi umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji ,ambapo alibainisha kuwa hali ya upatikanaji maji wa halmashauri ya Meru imebadilika kutokana na wananchi wengi kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya vyanzo vya maji
Alisema kuwa wao kama halmashauri Ili kukabiliana na tatizo hili wamejipanga kuanzisha operation ya utunzaji wa vyanzo vya maji ,ikiwemo upandaji miti ,kizuia watu wasijenge milimani wala kufika kuharibu vyanzo hivyo pamoja na kuhakikisha watu wanafata sheria ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo hivyo vya maji
Naye Kaimu mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la pangani Abrahamu Yesaya alisema kuwa wameanzisha ligi hii ikiwa ni agizo la waziri wa maji Juma Uweso ,ambapo alisema kuwa wametumka michezo hii kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji
Alisema kuwa katika ligi hizi jumla ya timu nane zilishiriki michezo Kwa mfumo wa ligi baadae zikaingia nusu fainali ambayo walicheza Kwa mtindo wa mtoano ambapi zilipatikana timu mbili ambayo Moja kutoka kata ya Mbunguni ijulikanayo kwa jina la Charity Fc na msitu wa mbongo Fc ambapo katika mchezo huu msitu wa mbongo Fc iliibuka mahindi Kwa kushinda penati tano Kwa tatu.
Alibainisha kuwa mashindano haya hayataishia apa wataendelea kufanya mara kwa mara kwani yatasaidia kuendelea kuwahamasisha wananchi kuendelea kutunza mazingira .