Mbunge wa bunge la Rwanda Gamariel Mbonimana ametangaza kujiuzulu baada ya kukumbwa na tuhuma za kuendesha gari akiwa amelewa.
Mbonimana ametangaza kujiuzulu huku akiomba msamaha kwa Rais Paul Kagame na kuapa kwamba ameamua kuacha kunywa pombe
Katika akaunti yake ya Twitter mbunge huyo alisisitiza zaidi kwamba atajitolea kutumikia jukumu lolote ambalo atapewa ikiwa Bw. Kagame ataona inafaa.
“Kutoka ndani ya moyo wangu, naomba radhi kwa Rais wa Jamhuri na umma kwa ujumla,” aliandika.
"Ilikuwa makosa kwangu kuendesha gari nikiwa nimekunywa pombe. Nimeamua kuacha pombe" aliandika katika mtandao wake wa Twitter
Social Plugin