Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VIDEO YA MAMA MJAMZITO KUFUMANIWA LIVE NA MMEWE AKICHOVYA ASALI NA MCHUNGAJI YAENDELEA KUZUA GUMZO MTANDAONI


Wanamtandao wamekuwa kwa siku kadhaa sasa wakiskia kuhusu maneno ya 'Martha Don't Move' kwenye mitandao.

Wengi wanajiuliza ni kipi kinaendelea kuhusu na binti huyu kwa jina la Martha.

Hata hivyo, 'Martha Don't Move' ni video moja iliyorekodiwa nchini Zambia na mwanaume aliyempata mkewe akichemsha damu na pasta.

Tukio hilo linaloaminika kutokea nchini Zambia linaonesha mwanaume mwenye nyumba akiingia katika chumba chao cha kulala na kwa mshangao mkubwa anamfumania mkewe mwenye ujauzito mkubwa akiwa uchi wa mnyama kitandani na mwanaume mwingine ambaye alikuwa anajiita mchungaji wa kanisa.

 Kwa mujibu wa video hiyo, mwanaume huyo alikuwa amearifiwa na mkewe kwamba anasafiri ila hakujua kuwa alikuwa na njama ya kupeana tunda lake la ndoa.

Baadaye anarudi nyumbani na kumpata peupe kwenye kitanda chao cha ndoa akijifurahisha na jamaa anayedaiwa kuwa mhubiri.

 Huku akiwa amejawa na hamaki, mwanaume huyo anatishia kufanya mabaya kwa mkewe kutokana na usaliti ambao ameshuhudia. 

Ni wakati huo ambapo mkewe anajaribu kumsogelea kumbembeleza aache kuwaka moto lakini hamaki inampanda.

"Martha don't move, don't . . . I will kill you, don't move (Martha usijaribu kunisogea, usinijaribu kabisa . . . Nitakuua ukicheza, usinisogelee Martha," mwanaume huyo alimuonya mkewe.

 Jamaa huyo alionekana kukerwa zaidi kuwa mkewe aliyeamua kupeana asali yake ndani ya chumba chao cha kulala. 

"Martha, Martha on my bed . . . on my bed Martha (Martha, unanifanyia haya kwa kitanda changu . . . kweli Martha unafanya katika kitanda changu," aliongeza. 

Kwenye video hiyo, mwanaume huyo anasema mkewe alikuwa amemuarifu kuwa anaenda eneo linaloitwa Kitwe kwa ajili ya kuitembelea familia yake kumbe alikuwa amepanga mengine.


Kwenye mtandao wa Twitter, kuna video ambayo imekuwa ikisambazwa ya mwanaume mmoja ambaye alimfumania mkewe mjamzito akiwa anakula uroda na mwanaume mwingine katika kitanda chao cha ndoa.


 Mumewe baada ya kumuaga aliondoka lakini ufika njiani alibadili mawazo na kurudi ambapo alipigwa na butwaa kile alichokiona kikitendeka chumbani mwake.


Si tu aliwafumania wakishiriki tendo la ndoa bali pia alipata vitu vinavyoaminika kuwa vya kishirikina vimetapakaa ndani mwa chumba chake cha malazi huku wawili hao wakiwa uchi.

Video iliyorekodiwa na mume huyo ambayo imesambaa mitandaoni, inaonyesha mume akimwambia mke huyu asisogee, kwamba atamuua.

Mke akiwa bado uchi alijaribu kumsihi mumewe, huku mchungaji akishindwa kujikwamua na kuharakisha kuvaa kaptula yake ili kuficha uchi wake.


Tukio hilo lilikuwa la kustaajabisha kwani mchungaji aliyetajwa, ili kuogofya kivuli cha mume wa Martha au kufanya chumba kuwa cha kimapenzi alikuwa amepamba chumba kwa mishumaa, maua na vitu vingine vilivyokuwa sakafuni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com