Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAKUKURU YABAINI MAPUNGUFU BAADHI YA MIRADI YA MAENDELEO KAGERA


Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera Bw. John Joseph akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa ofisi za Takukuru.


Na Mbuke Shilagi Kagera.


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imebaini mapungufu katika baadhi ya miradi ya maendeleo wakati wa zoezi la ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi hiyo katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa.


Akizungumza na vyombo vya habari leo Novemba 02,2022 katika ukumbi wa ofisi za Takukuru, Mkuu wa Takukuru Bwa. John Joseph amesema kuwa wamefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo 48 yenye thamani ya zaidi ya Bilion 16 ambayo ni ujenzi wa mradi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa mradi wa maegesho ya magari makubwa, mradi wa miundo mbinu ya maji, ujenzi wa vituo vya Afya na Zahanati pamoja na ujenzi wa vyoo na kubaini mapungufu kwa baadhi ya miradi hiyo.


Na kwamba mapungufu hayo yamekuwa ya kutumia vifaa vyenye ubora tofauti na ilivyo elekezwa katika BOQ, utoaji wa LPO kwa baadhi ya wazabuni bila kuonesha idadi halisi ya vifaa vinavyotakiwa kununuliwa pamoja na vifaa kutolewa stoo bila kurekodiwa.


Pia wamebaini uwepo wa urushwaji wa bei kwa baadhi ya vifaa kuliko bei ya soko pamoja na kubaini baadhi ya wazabuni wa miradi kupewa malipo ya awali hawakuwa wameanza kazi na kutokuwepo katika maeneo ya miradi.


Aidha ameongeza kuwa miradi hiyo 48 iliyofanyiwa ufuatiliaji imeonekana miradi 31 haikuwa na kasoro na hivyo inaendelea kukamilishwa na baadhi imekamilika huku miradi saba yenye thamani ya zaidi ya Bilion nne imeanzishiwa uchunguzi wa kina.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com