Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia mkazi wa Nyombo Tarafa ya Lupembe wilayani Njombe, Adelina Ngollo (36) kwa tuhuma za kuwachoma moto watoto wake wawili na kuwasababishia madhara makubwa.
Mwanamke huyo anadaiwa kuwachoma watoto hao ambao mmoja ana umri wa miaka (4) na mwingine (7) kutokana na tabia yao ya kwenda kwa majirani na kuombaomba chakula.
Inaelezwa kuwa baada watoto hao kuwa na tabia hiyo majirani walimuita mwanamke huyo na kumueleza kuwa malezi ya watoto hao siyo mazuri, maneno hayo yalimuumiza na kuyaweka moyoni.
Via Mwananchi
Social Plugin