Juma Homera, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amealiagiza Jeshi la Polisi mkoani humo, kufanya uchunguzi wa haraka kuwabaini watu waliohusika na tukio la kufukua mwili wa mwanamke Neema Mlomba na kunyofoa baadhi ya viungo vyake ikiwemo moyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea Kijiji cha Luteba Halmashauri ya Busokelo ambapo marehemu alifariki akiwa na umri wa miaka 26.
Homera akataja viungo vilivyonyofolewa kwenye mwili wa Neema na watu wasiojulikana na kuhusisha vitendo hivyo na imani za kishirikina.
Mtoto wa marehemu yuko hospitali ya Wazazi Meta chini ya uangalizi maalum wa madaktari akiendelea kupatiwa huduma za matibabu.
Via EATV
Social Plugin