Polisi nchini India imewatupia lawama Panya kwa kutafuna kilo 200 za Bangi
KWA mujibu wa taarifa kutoka nchini India, Polisi wamewalaumu panya kwa kuharibu karibu kilo 200 za bangi iliyokamatwa kutoka kwa wauzaji na kuhifadhiwa katika vituo vya Polisi.
“Panya ni wanyama wadogo na hawana hofu na Polisi. Ni vigumu kulinda dawa dhidi yao,” Mahakama katika jimbo la Uttar Pradesh imesema.
Mahakama iliwataka Polisi kuwasilisha dawa hizo kama ushahidi katika kesi za uuzaji na ununuaji wa dawa za kulevya.
Hakimu alitaja kesi tatu ambapo bangi iliharibiwa na panya.
Jaji Sanjay Chaudhary alisema katika agizo kwamba Mahakama ilipowataka Polisi kuwasilisha dawa hiyo iliyokamatwa kama ushahidi, iliambiwa kuwa kilo 195 za bangi “ziliharibiwa” na panya.
Social Plugin