TRA SHINYANGA YAZINDUA WIKI YA SHUKRANI KWA MLIPA KODI....WAJIVUNIA KUKUSANYA KODI KWA HIARI JUU YA VIWANGO

Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga, wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph, Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom), Shule ya Sekondari Old Shinyanga na wadau wakiandamana kutoka Ofisi za TRA, kupitia mitaa mbalimbali Mjini Shinyanga kuelekea Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Awali Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika Ofisi za TRA wakijiandaa kuanza maandamano kuelekea kwenye Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga. 
Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga na wadau wakiandamana kutoka Ofisi za TRA kuelekea Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mapato Tanzania (Tanzania Revenue Authority – TRA) Mkoa wa Shinyanga imezindua Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga huku ikijivunia mafanikio ya kukusanya kodi shilingi Bilioni 12.4 sawa na asilimia 103% juu ya malengo waliyojiwekea ya kukusanya shilingi Bilioni 12 katika kipindi cha Mwezi Julai hadi Oktoba,2022.

Uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi ikiongozwa na Kauli mbiu ya "Asante kwa kulipa kodi kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa ; Kazi Iendelee" umefanyika leo Jumatano Novemba 23,2022 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.

Uzinduzi huo umetanguliwa na maandamano ya wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga, wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph, Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom), Shule ya Sekondari Old Shinyanga na wadau mbalimbali kuanzia Ofisi za TRA Mjini Shinyanga kupitia mitaa mbalimbali na kuhitimisha maandamano hayo kwenye Uwanja wa Zimamoto uliopo Nguzo Nane Mjini Shinyanga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara (TCCIA) Mkoa wa Shinyanga, Jonathan Kifunda Manyama ameipongeza TRA Mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kukusanya Kodi kistaarabu huku akiwashukuru wananchi kuendelea kulipa kodi na kuwezesha TRA kukusanya kodi kwa viwango vinavyotakiwa.

Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Mdesa amesema wanajivunia mafanikio makubwa katika ukusanyaji kodi kwa hiari kutoka kwa wafanyabiashara akitolea mfano katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Oktoba 2022 wamekusanya kodi kiasi cha Shilingi Bilioni 12.4 sawa na asilimia 103% ikiwa ni juu ya malengo waliyojiwekea ya kukusanya shilingi Bilioni 12 katika kipindi hicho.

Mdesa amewashukuru wafanyabiashara kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari.

“ Katika wiki hii ya Shukrani kwa mlipa kodi, tutatoa tuzo kwa taasisi, makampuni na watu binafsi, ambao wamefanya vizuri katika ulipaji wa kodi. Pia maafisa wa idara mbalimbali za TRA watatoa elimu na kujibu maswali mbalimbali ya wananchi kuhusu masuala ya kodi.

“Pia maafisa wa TRA watafanya shughuli mbalimbali zinazolenga kuhamasisha umuhimu wa ulipaji wa kodi, pamoja na kutoa misaada kwa taasisi mbalimbali zenye uhitaji. TRA mkoa wa Shinyanga itatoa zawadi kwa walipakodi waliofanya vizuri, kupitia sherehe za kilele cha wiki ya shukrani kwa mlipakodi hapa katika uwanja wa Zimamoto siku ya Ijumaa Novemba 25,2022 kuanzia saa 3:00 asubuhi ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema”,amesema Mdesa.

Kwa upande wake, Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi amesema TRA inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria huku akiwaomba wananchi kuwa wazalendo kwa kutambua umuhimu wa kulipa kodi, kwa kuwa fedha zinazokusanywa zinaisaidia serikali kutekeleza mipango mbali mbali ya maendeleo.

TAZAMA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara (TCCIA) Mkoa wa Shinyanga, Jonathan Kifunda Manyama akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Mdesa , kulia ni Meneja wa TRA Msaidizi - Madeni Mkoa wa Shinyanga, Estomih Mossi na Meneja wa TRA Msaidizi Ukaguzi Mkoa wa Shinyanga, David Mkwabe (kulia). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara (TCCIA) Mkoa wa Shinyanga, Jonathan Kifunda Manyama akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Mdesa , kulia ni Meneja wa TRA Msaidizi - Madeni Mkoa wa Shinyanga, Estomih Mossi na Meneja wa TRA Msaidizi Ukaguzi Mkoa wa Shinyanga, David Mkwabe (kulia).
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Mdesa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi akifuatiwa na Meneja wa TRA Msaidizi Ukaguzi Mkoa wa Shinyanga, David Mkwabe na Meneja wa TRA Msaidizi - Madeni Mkoa wa Shinyanga, Estomih Mossi
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Mdesa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga. 

Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga. 

Meneja wa TRA Msaidizi Ukaguzi Mkoa wa Shinyanga, David Mkwabe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga. 
Katibu Msaidizi wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo  akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga. 
Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika Ofisi za TRA wakijiandaa kuanza maandamano kuelekea kwenye Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga. 

Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga, wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph, Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom), Shule ya Sekondari Old Shinyanga na wadau wakiandamana kutoka Ofisi za TRA, kupitia mitaa mbalimbali Mjini Shinyanga kuelekea Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga, wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph, Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom), Shule ya Sekondari Old Shinyanga na wadau wakiandamana kuelekea Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga na wadau wakiandamana kutoka Ofisi za TRA kuelekea Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga na wadau wakiandamana kutoka Ofisi za TRA, kupitia mitaa mbalimbali Mjini Shinyanga kuelekea Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.

Wafanyakazi wa TRA wakitoa burudani ya kucheza muziki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga
Wananchi wakitoa burudani ya kucheza muziki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga

Mwananchi akijibu swahili kuhusu TRA wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa TRA wakiwa kwenye uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga

Mgeni rasmi na maafisa wa TRA wakipiga picha na wananchi kwenye uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga

Mgeni rasmi na maafisa wa TRA wakipiga picha na wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph kwenye uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga
Mgeni rasmi na maafisa wa TRA wakipiga picha na wanafunzi wa shule ya Sekondari Old Shinyanga kwenye uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga
Mgeni rasmi na maafisa wa TRA wakipiga picha na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom) kwenye uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga
Mgeni rasmi akipiga picha na maafisa wa TRA mkoa wa Shinyanga kwenye uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga
Mgeni rasmi akipiga picha na wafanyakazi wa TRA mkoa wa Shinyanga kwenye uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga
Mgeni rasmi akipiga picha na wafanyakazi wa TRA mkoa wa Shinyanga kwenye uzinduzi wa Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post