Na Mwandishi Wetu , SHINYANGA
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa, ametaja majina ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambayo yamepitishwa na Halmashauri kuu ya CCM Taifa.
Akizungumza kwa njia ya simu akitokea Dodoma, amewataja waliopitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga kuwa ni Mabala Mlolwa ambaye anatetea kiti chake kwa awamu nyingine tena, Mwingine ni Costantine Mollo Nkuba na Eneza Onel Kanuya.
Nafasi ya ujumbe wa wa halmashauri kuu ya CCM taifa (NEC) waliopitishwa ni Gasper Hanson Kileo ambaye anatetea nafasi yake kwa mara nyingine, mwingine ni Nyachiro Maiga Magongo na Majuto Clement Manyilizu.
Social Plugin