Wanyama ambao mbinu zao za kuwinda na kuepuka kuwindwa ni za kipekee sana hivi kwamba wapinzani wao huachwa wakiwa hoi.
Kindi wa Carlifornia
Mnyama huyu mdogo anakabiliwa na matatizo makubwa. Mandhari anayoishi yenye miamba na korongo zenye kina kirefu ni kawaida kwa aina hii ya wanyama wanaoishi katika misitu huko California, Oregon magharibi, na Nevada ya magharibi nchini Marekani. Lakini kutokana na hali ya wazi ya nyumba zao, wao daima wako katika hatari ya kudhulumiwa.
Adui mmoja ni nyoka nyoka kayamba ambaye huwinda kwa kunusa na, mara moja anapokupata kwenye njia, huwezi kumuepuka .
Lakini kindi wa ardhini huko California wana njia ya busara ya kudanganya adui yake. Wamejifunza kuficha harufu yao kwa kutumia meno ya sumu ya nyoka kayamba ambyo hujificha nayo
Utaratibu huu unafikiriwa kuwa funzo kwa chindi na kutoka kizazi kimoja hadi chengine kizazi na harufu hii ni muhimu kwa hindi yeyote kuepuka nyoka.
Pundamilia: 'Kwa nini pundamilia wana mistari?'
Punda milia
Swali hili, mojawapo ya kongwe zaidi katika biolojia ya mabadiliko, limesumbua wanasayansi tangu Charles Darwin na Alfred Russell walipolijadili kwa mara ya kwanza. Lakini kulingana na utafiti wa kisasa, wanyama hawa hutumia mistari hiyo ili kujificha na kujilinda dhidi ya maadui wanapotoroka.
Lakini hii inawezaje kuwa wakati mistari hii inaifanya ionekane kuwa maarufu zaidi? Jibu ni siri ya hila yoyote yenye nguvu zaidi ya mchawi: udanganyifu wa macho.
Nyeusi na nyeupe ni rangi ambazo, zikichanganywa pamoja, zinaweza kucheza michezo mingi kwa akili na mara nyingi kwa macho ya wanyama.
Dkt. Martin Howe wa Chuo Kikuu cha Bristol amekuwa akisomea maono ya chui na dumaw. Anasema: 'Nimekuwa nikichunguza uwezo wao wa kuona wanyama wengine kwa miaka kadhaa na ninapendezwa sana na kile kinachoathiri macho ya mwindaji wa pundamilia mwenye mistari.'
Walichunguza iwapo punda milia hawa huwadanganya wanyama wanaokula wenzao kupitia 'udanganyifu wa gurudumu la gari'. Katika hili, wakati kitu kinachosonga kwa kasi kama gurudumu kinapokuja mbele yako, ubongo hurahisisha kuelewa.
Lakini kwa njia hii akili haielewi kabisa mwelekeo wake. Ndiyo maana tunapoona magurudumu ya gari au mabawa ya ndege yakienda kwa kasi, tunafikiri kwamba yanasonga polepole au kuelekea upande mwingine.
Utafiti wa Howe ulionyesha kuwa kundi la pundamilia wanapotembea pamoja, michirizi yao inaleta dhana potofu ya 'dizeli inayotembea'. Howe anaamini kwamba mwindaji anapoona msogeo wa michirizi hii, anadhani pundamilia wanasogea upande wa kushoto wakati wanaweza kuwa wanahamia kulia.
Kila muda una thamani katika uwindaji, lakini pundamilia hufanikiwa kutoroka kwa kutumia fursa hii na hivyo kudanganya Wanyama wengine.
Cuttle fish
Samaki aina ya cuttlefish
Samaki aina wa Cuttlefish wamejenga ulinzi wa busara ili kuepuka kuliwa ambao pia ni mzuri kutazama. Badala ya kujificha kwenye gamba gumu , anatumia rangi ya mazingira yake kujificha .
Samaki huyo ana viungo vidogo kwa jina chromotophores katika tabaka la nje la ngozi yao. Anaposogea, kila kromatophore hutoka katika ubongo na misuli na ghafla hubadilika kuwa mduara wa rangi.
Huku mamilioni ya chromatophore kama hizo zikifanya kazi kwa wakati mmoja, cuttlefish huunda ruwaza za rangi mahususi zinazochanganyika popote. Pia, sura na muundo wake unaweza kubadilika sana hivi kwamba ikaonekana kuwa ametoweka kabisa.
Ujanja huu wote unashangaza zaidi kwa sababu cuttlefish wenyewe hawawezi kuona rangi yoyote. Kwa hiyo ikiwa haoni rangi zote anazoiga, anafanyaje hivyo kwa usahihi?
Utafiti mpya umefichua siri ya samaki huyu. Seli zao za ngozi zina protini inayoitwa opsin, ambayo pia hupatikana kwenye retina ya jicho. Kwa hivyo ngozi yao inaweza 'kuona' rangi yenyewe kupitia seli hizi za kugundua mwanga, ndio maana aenaweza kusekana kuwa na mojawapo ya ngozi nzuri na zenye akili zaidi ulimwenguni.
Simba wa Afrika
Simba
Ikiwa mnyama anafanana na simba na wengine wanafikiri ni simba, unaweza kufikiri hivyo, lakini si lazima iwe hivyo. Eneo la Okavango Delta nchini Botswana ni makao ya simba jike wachache ambao manyoya yao mazito na miungurumo kama ya simba mara nyingi huwachanganya wapinzani.
Mmoja wa simba hawa wa kike wasio wa kawaida ni Mamoriri, ambaye anaonekana na ana sauti kama ya simba dume, lakini kwa hakika ni simba jike.
Sawa na simba wengine wa kike wenye nywele nyingi, Mamoriri anaaminika kuwa na mabadiliko ya homoni kutokana na mabadiliko katika jeni zake. Kwa hivyo anaonekana kama simba dume.
Katika simba, wanaume ndio wanaotetea maeneo yao kutoka kwa wapinzani, ambayo familia nzima humtegemea. Kwa sababu mamuriri wanaonekana kama wanaume, wanaume wapinzani wanaotaka kuvamia eneo lao watafikiria mara mbili kabla ya kutekeleza uvamizi .
Ikiwa kikundi cha Mamoriri kinaweza kupanua eneo lake kwa sababu ya kutokuelewana huku, kinaweza pia kuhakikisha usalama na maisha ya simba hawa. Mabadiliko haya ya jeni yamezaa aina mpya na ya kusisimua ya utunzi.
Kivunja njugu{Mantis}
Mantis
Misitu ya Malaysia sio tu nyumbani kwa wadudu wengi wenye mabawa, lakini pia wanyama wanaowinda wanyama wengine ambao huchukua fursa yao. Hii ina maana kwamba ikiwa wadudu hawa watakwepa kuliwa, inabidi wawe na kasi ya umeme ili wasiweze kukamatwa kwa urahisi.
Lakini wakiepuka taya za wanyama wanaowinda wanyama wengine, wadudu hawa hawawezi kukaa mbali na maua ya rangi ambayo nekta na juisi hupendwa.
Mantis wa orchid hujifunika mwili wao wote kwa ufichaji mzuri na wa kuvutia. Kwa macho yao makali , mantis hawa ni kati ya wanyama wanaowinda kwa ujanja na hatari zaidi duniani, wanapojificha na kuonekana kuwa maua.
Lakini 'ua hili bandia' lina sifa nyingine. Anapaswa kula kila baada ya siku mbili kwa sababu hawezi kusubiri kwa muda mrefu kama maua.
Tangu wanasayansi wa mambo ya asili walipogundua spishi hiyo katika karne ya kumi na tisa, wameshuku siri ya kufaulu kwa wadudu hawa, hasa kwa vile ni maarufu zaidi kuliko ua wanaloiga.
Kwa kuwa wadudu huvutiwa na mvuto wa ua la kuvutia, Mantis huwa na mwonekano wa kuvutia zaidi kuliko ua halisi na vilvile pia huwa na rangi angavu zaidi.
Mara tu mdudu anaponaswa katika mtego huu, inakuwa vigumu kutoroka.
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin