Lazaro Adamson (40) mkazi wa Kaloleni wilayani Songwe, anashikiliwa na polisi mkoani Songwe kwa kumuua Berta Shugha (69), na kisha kuukata kata mwili wake vipande vipande na kuuchoma na kuanza kuula kama mishikaki.
Mkuu wa wilaya hiyo Simon Simalenga amesema mtuhumiwa alidai kwamba alimuua mwanamke huyo kwa kumpiga panga kisogoni na katikati ya kichwa na kwamba alipopoteza maisha ndipo akaanza kumkata kata.
"Alisema baada ya kumuua alimkata nyayo za miguu yote, akatoa utumbo na kuukamulia kwenye beseni na yeye anadai kuwa alianza kula kwa vile alikuwa na hamu ya nyama," amesema DC Simalenga.
Aidha awali baadhi ya viungo vya marehemu havikujulikana vilipo na baadaye vilipatikana "Baadhi ya viungo ambavyo vilikuwa havionekani kama vile mapaja, hatimaye Askari wetu wa Jeshi la Polisi wamevipata vikiwa vimefichwa katika shimo la choo ambacho kilikuwa hakitumiki, viungo hivyo vimepatikana vikiwa vimechomwa na katika hali ya kushangaza mtuhumiwa alianza kula nyama hiyo mbele ya Askari," ameongeza Simalenga.
Wakizungumzia tukio hilo ambalo limetokea usiku wa Novemba 13, 2022, Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Chang’ombe walisema walishtukia uwepo wa mauaji hayo baada ya kuona damu nyingi zikiwa zimezagaa kwenye nyumba ya mtuhumiwa, jambo ambalo halikuwa la kawaida.
Via: EATV
Social Plugin