*********************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba Sc leo imeingia uwanjani kumefanyana na timu ya Singida Big Star mechi ambayo Simba Sc ikilazimisha sare ya 1-1 baada ya kusawazisha bao kipindi cha pili.
Singida Big Star walianza kupata bao kupitia kwa nyota wao Deus Kaseke akipokea krosi kutoka kwa Hamisi Ndamla katika dakika za mwazo kipindi cha kwanza.
Mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Liti Mkoani Singida, timu ya Singida Big Star ilionesha kutawala mpira kipindi cha kwanza huku wakishambulia kwa kushtukiza ndipo wakapata bao la mapema.
Simba Sc iliwapumzisha baadhi ya mastaa wake akiwemo Okra pamoja na Manula huku Kakolanya akiaminiwa langoni.
Social Plugin