Kijana Richard Mtafya maarufu kama Masumbuko mwenye umri wa miaka 19, mkazi wa Ludewa kijijini inadaiwa amejiua kwa kunywa maji ya betri kwa kukwepa mkono wa sheria kwa shtaka la mauaji lililokuwa likimkabili.
Kwa mujibu wa mtendaji wa Kijiji cha Ludewa Kijijini Atanas Mtega pamoja na Baraka Haule ambaye ni Katibu wa Kitongoji cha Ngongano wamesema kuwa kabla ya kifo chake mnamo Novemba 14 mwaka huu kijana huyo kwa kushirikiana na mwenzake walifanya mauaji ya kijana mwenzao aliyefahamika kwa jina la Alfred kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.
Aidha kwa upande wake mke wa marehemu huyo Angela Mhagama, amekiri kuwa alikuwa na mawasiliano na kijana huyo aliyeuawa na mumewe huku akieleza kilichotokea baada ya mumewe huyo kuona mawasiliano yao.
Magreth Haule ni bibi wa marehemu huyo ambaye pia ni mlezi wa kijana huyo toka alipokuwa mtoto mdogo amesema wakati matukio hayo yanatokea alikuwa shambani huku wananchi wakielezea masikitiko yao juu ya tukio hilo.
Via: EATV
Social Plugin