HAKIRASILIMALI WAENDESHA JUKWAA ZA UZIDUAJI, UWAZI, UWAJIBIKAJI SEKTA YA UZIDUAJI, MADINI, MAFUTA NA GESI ASILIA


Mkurugenzi mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony akizungumza kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji Jijini Dodoma.

Na Marco Maduhu, DODOMA

TAASISI ya HakiRasilimali imeedesha jukwaa la uziduaji na kukutanisha washiriki takribani 200 kutoka Sekta ya Uziduaji Madini, Mafuta na Gesi asilia.

Jukwaa hilo limefanyika leo Novemba 24, 2022 Jijini Dodoma, ambalo litakwenda hadi kesho, na limekutanisha washiriki kutoka Serikali kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Asasi za Kiraia, Makampuni ya madini, Wachimbaji wadogo, wawakilishi katika Jamii, wanataaluma, na waandishi wa habari.

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony akifungua jukwaa hilo, amesema kila mwaka hukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya uziduaji kujadili kwa kina, kubadilisha uzoefu na kujifunza kutoka kwa washiriki namna ya kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta.

“HakiRasilimali inaamini kuwa uwazi na uwajibikaji katika sekta ya uziduaji yani Madini, Mafuta na Gesi asilia ndiyo chachu ya maendeleo ya sekta na taifa kwa ujumla,”amesema Anthony.

“Dhamira ya HakiRasilimali katika kuhimiza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya uziduaji inasukumwa na changamoto tunazoziona katika sekta, na lengo letu ni kuhakikisha haki za wanachi wanaoishi katika maeneo husika zinalindwa, Serikali inapata manufaa stahiki, lakini pia mazingira ya uwekezaji yanaendelea kuwa Rafiki na kuvutia uwekezaji,”ameongeza.

Aidha, wakati mjadala wa Siasa za kijiographia zinazohusu sekta ya uziduaji, lilizungumzwa suala la Watanzania kunufaika na Rasilimali zao, ambapo Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Josephine Lemoyan, amesema ili Rasilimali  zipate kunufaisha wazawa ni lazima iwepo mifumo mizuri ya usimamizi wa Rasilimali.

“Huwa naumia ninapoona Rasilimali zetu hazinufaisha Watanzania na ninaiomba Serikal iweke mifumo mizuri ya usimamizi wa Rasilimali zetu ili tunufaike nazo vizazi na vizazi,"amesema Lemoyan.

Nao Wachimbaji wa madini akiwamo Mary James, wameiomba pia Serikali itunge sera nzuri ambayo itasaidia Watanzania kunufaika na Rasilimali za nchi yao, pamoja na kusaidia wachimbaji wadogo wapate mikopo.

Naye Veronica Zano kutoka Oxfam nchini Zimbabwe, amesema ili Rasilimali zipate kunufaisha Afrika ni lazima pia kuwe na Sera ya pamoja.

Aidha, Katika Jukwaa hilo la Sekta ya uziduaji zimejadiliwa mada mbalimbalimbali ikiwamo ya Siasa ya Kijiographia katika sekta ya uziduaji, kuhama kwenye Nishati ya Zamani kwenda Nishati Safi, Sheria za Madini na uvutiaji wawekezaji, na ushirikishwaji wa wanawake katika sekta ya uziduaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony akizungumza kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya HakiRasilimali Donald Kasongi akizungumza kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Josephine Lemoyan akizungumza kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Uwasilishaji wa Mada ukiendelea kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Uwasilishaji wa Mada ukiendelea kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Uwasilishaji wa Mada ukiendelea kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.
 Uwasilishaji wa Mada ukiendelea kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Wadau wa sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la uziduaji wakisikiliza uwasilishwaji wa mada mbalimbali.

Jukwaa la sekta ya uziduaji likiendelea.

Jukwaa la sekta ya uziduaji likiendelea.

Jukwaa la sekta ya uziduaji likiendelea.

Jukwaa la sekta ya uziduaji likiendelea.

Jukwaa la sekta ya uziduaji likiendelea.

Jukwaa la sekta ya uziduaji likiendelea.

Jukwaa la sekta ya uziduaji likiendelea.

Jukwaa la sekta ya uziduaji likiendelea.

Jukwaa la sekta ya uziduaji likiendelea.

Mdau wa sekta ya uziduaji Clay Mwaifwani kutoka Timu ya wanasheria watetezi wa mazingira kwa vitendo (LEAT) akichangia mada kwenye jukwaa la uziduaji.

Uchangiaji mada ukiendelea kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Uchangiaji mada ukiendelea kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Uchangiaji mada ukiendelea kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.
wadau wakiwa kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post