Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWALIMU MADRASA KAHAMA ADAIWA KULAWITI WATOTO 10 AKIWARUBUNI KUWAPATIA SHILINGI 1,500



Na Mwandishi Wetu, KAHAMA

Mwalimu wa madrasa ya shunu anayejulikana kwa jina la Faidh ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka (20-25) mkazi wa Shunu Kata ya Nyahanga Wilaya Kahama anadaiwa kulawiti watoto kumi, wanaosoma madrasa katika msikiti wa Mohamed Shunu ambapo inasemekana aliwalawiti watoto hao kwa nyakati ntofauti kwa kuwarubuni kwa kuwapa pesa Sh.1500 kisha kuwafanyia ukatili huo.

Akieleza juu ya tukio hilo jana Mwenyekiti wa Mtaa wa shunu, Joseph Kaliwa amesema kuwa siku ya ijumaa alipata taarifa ya tukio la kulawitiwa watoto hao, hali iliyomfanya kuitisha kikao cha wazazi wa watoto waliofanyiwa ukatili huo pamoja na Afisa ustawi wa jamii Wilayani humo kisha wakawapeleka  hospitali kwaajili ya kupatiwa dawa itakayosaidia kuwakinga na magonjwa.


Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,Janeth Magomi, Amekiri kutokea kwa tukio hilo la kulawitiwa watoto hao 10.


"Nathibitisha kutokea kwa tukio hili ambalo lililotokea Katika Mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga Wilaya Shinyanga ambapo sisi kama jeshi la polisi tulifika eneo la tukio na kujionea ni kweli watoto hao wamelawitiwa na tuliwapeleka hospitali na mtuhumiwa tumemkamata ambapo awali walikuwa wametoroka na kukimbilia Kigoma,"amesema Magomi.


"Jeshi la polisi mkoa shinyanga linatoa wito kwa wananchi wawe wanatoa taarifa haraka,ili kuwanusuru watoto wetu sambamba na kuwapa hukumu kali wale wanaokiuka sheria"Ameongeza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com