Msichana moja mchanga amemtia babake wasiwasi baada ya kurejea kutoka shuleni kila siku akilia.
Msichana huyo alilalamika kuwa amekuwa akikumbana na matatizo shuleni kwani wanafunzi wenzake hawampendi na kila mara wanamtoroka.
Kulingana na Dexterouz11 kwenye Twitter, baba huyo aliamua kukabiliana suala hilo kwa kutembelea shule hiyo ambapo alizungumza na wanafunzi wenzake waliothibitisha ripoti za bintiye.
Wanafunzi wenzake walifichua kwamba walikuwa wakimtenga msichana huyo mdogo kwa sababu alikuwa mkaidi na mwalimu wao aliwaagiza waepukane naye.
"Huyu jamaa aliniambia kuhusu mtoto wake anayerudi nyumbani kila mara kulalamika kuwa kila mtu anamchukia shuleni. Alimfuata shuleni ili kujua tatizo na wanafunzi wakasema hawaongei naye kwa sababu mwalimu wao aliwaambia wamuepuke."
Walipokabiliwa, mwalimu huyo alisema kuwa binti wa jamaa huyo alikuwa mkaidi na hiyo ndiyo njia pekee ya kukabiliana na kiburi chake.
Mwalimu ambaye aliwaagiza wenzake kumuepuka alisema ilikuwa njia bora ya kumrekebisha. Maelezo yanaonyesha kuwa baba huyo aliyekasirika alizua tafrani hivi kwamba shule ilimfukuza kazi mwalimu huyo muda mfupi baadaye.
Social Plugin