KATIBU Mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 19,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya kumtaka aliyekuwa katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ali Kakurwa kujitathini na kuomba radhi wananchi na Viongozi kwa ujumla kutokana na video yake aliyoitoa Mtandaoni.
..................................
Na Alex Sonna-DODOMA KATIBU Mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi,amemtaka aliyekuwa katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ali Kakurwa kujitathini na kuomba radhi wananchi na Viongozi kwa ujumla kutokana na video yake aliyoitoa Mtandaoni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 19,2022 jijini Dodoma Kihongosi amesema kuwa maneno aliyotumia si rafiki, si ya kiungwana, yamejaa ukakasi na yamelenga kuchonganisha Serikali na wananchi hasa wakulima.
Dk.Bashiru alitoa maneno ya kuchinganisha Serikali na wananchi wakati akihutumia mkutano wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) mjini Morogoro kwamba viongozi hawapaswi kusifiwa kuwa ‘anaupiga mwingi’ wanapotekeleza majukumu
“Ninamtaka Dkt.Bashiru ajitathimini na kuwaomba radhi watanzania na Serikali kwa ujumla kutokana na kauli yake chonganishi ambayo imeonekana sio nzuri ikizingatiwa yeye alishawahi kuwa kiongozi na alikuwa akiipongeza Serikali Kwa mazuri inayoyafanya " amesema Kihongosi
Amesema kuwa wao kama UVCCM hawakubaliani na jambo hilo na serikali ya awamu ya sita inafanya kazi kubwa ambayo imekwenda kuacha alama katika eneo la wakulima, katika suala hilo tunaweza kutizama kipindi hicho bei ya mbolea ilipanda bei sana na ongezeko lile ilipelekea Rais Samia Suluhu Hassan kutoa ruzuku ya Sh.Bilioni 150 ili kupunguza bei ambayo ilikuwa Sh.130,000.
Kihongosi amesema kuwa serikali imeweka utaratibu na wakulima wananunua kwa bei nafuu jambo ambalo limegusa maisha yao na uchumi wa nchi.
“Sasa anapotokea kiongozi ambaye alikuwa na dhamana kubwa anatoa maneno yenye ukakasi kwamba viongozi hawapaswi kupongezwa bali wanapaswa kutolewa matamko ya kuwashinikiza hii sio sawa, nitoe rai kwa viongozi wa tabia hii sio njema.”amesisitiza
Aidha ameeleza kuwa Dk. Bashiru ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo na anajua kila kilichofanyika kwenye sekta hiyo na namna bajeti ilivyoongezeka katika mwaka huu wa fedha lakini anapofikia kutoa kauli hiyo ni jambo la kushangaza.
Social Plugin