Maafisa wa upelelezi katika Kaunti ya Kiambu wameanzisha uchunguzi katika kifo tatanishi cha afisa wa polisi mwanamke katika kituo cha polisi cha Kiandutu katika kaunti ndogo ya Thika Magharibi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, afisa huyo alijiua kwa kujipiga risasi kifuano mwendo wa saa nne kasorobo asubuhi mnamo Ijumaa - Novemba 25,2022.
Afisa mwenzake wa polisi ambaye aliripoti kisa hicho alishtuka baada ya kusikia mlio mkubwa wa sauti kutoka kwa nyumba ya mwendazake.
Afisa huyo aliambia afisa wa anayesimamia kituo hicho (OCS) ambaye alifika eneo la kituo akiwa na maafisa wenzake wa polisi.
Maafisa wenzake wa polisi wamesikitishwa na kisa hicho wakisema kuwa mwenzao hakuwa na dalili zozote za msongo wa mawazo.
Wenzake hata hivyo walisema kuwa alikuwa ameandika ujumbe ficche kwenye status yake ya WhatsApp usiku wa Alhamisi - Novemba 24. Ripoti ya polisi inasema kuwa ujumbe huo ulisema kuwa "kwa sababu kesho labda haiwezi kuwa yangu" na kuongeza wimbo "Sweet bye-bye".
Chanzo - Tuko News
Social Plugin