Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NDALICHAKO AMPONGEZA PROF MJEMA WA CBE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu kwenye mahafali ya 57 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako akikata utepe kuzindua jingo la maktaba la Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kabla ya mahafali ya 57 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salam ambapo wahitimu 1,065 walitunukiwa vyeti vya ngazi mbalimbali.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza kwenye Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), katika mahafali ya 57 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salam ambapo wahitimu 1,065 walitunukiwa vyeti vya ngazi mbalimbali. Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe akizungumza kwenye mahafali ya 57 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), leo Jumamosi
Sehemu ya wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE wakiwa kwenye mahafali yao leo Jumamosi

*********************

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imevitaka vyuo kuzingatia mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi vyuoni ili kuondoa malalamiko kutoka kwa waajiri kwamba wahitimu wengi wanahitimu bila kuwa na ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, wakati akizungumza kwenye mahafali ya 57 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salam ambapo wahitimu 1,065 walitunukiwa vyeti vya ngazi mbalimbali.

Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha na mafunzo mengi kufanyika kwa madharia bila vitendo na alipongeza chuo cha CBE kwa kuanzisha program ya uanagenzi ambapo mwanafunzi anasoma nusu ya masomo chuoni na nusu akiwa sehemu ya kazi.

“Malalamiko ni kwamba wahitimu wengi wanatoka vyuoni wakiwa na ujuzi ule ambao siyo unaohitajika kwenye soko la ajira na soko linahitaji rasilimali kazi ambayo vyuo havitoi kwa ukamilifu wake kutokana na kukosekana kwa mafunzo ya vitendo,” alisema

“Ndiyosababu naipongeza CBE kwa kuanzisha program ya uanagenzi ambayo mwanafunzi anakua darasani kwa asilimia 50 na anakuwa sehemu ya kazi kwa asilimia 50 na kwa kufanya hivi unatatua changamoto iliyokuwepo ya kuwa na wahitimu ambao hawana ujuzi sawasawa,” alisema

Alipongeza pia kuanzishwa kwa program atamizi kutoa nafasi kwa vijana kuatamia ujuzi wao kwamba vyuo vingine kama Mzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) vimeshaanzisha program kama hizo.

Alisema kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inatoa mafunzo ya uanagenzi ili kuhakikisha kama kuna kitu kimepungua kwa mwanafunzi kabla ya kuhitimu anapata ujuzi kwa vitendo kwa udhamini wa serikali.

Alisema serikali katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 ilitenga Sh bilioni 9 ambazo ziliwezesha vijana zaidi ya 62,000 kupata mafunzo ya uanagenzi na katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 kwaajili ya kuendelea kutoa mafunzo ya uanagenzi.

Alimpongeza Profesa Emmanuel Mjema kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa mkuu wa chuo hicho kwa kipindi cha miaka 10 kwani chini yake chuo kimepata mabadiliko makubwa kitaaluma kwani alikipokea kikiwa katika hali mbaya.

“Wanafunzi mmefanya kazi nzuri sana kufaulu mitihani yenu na pia napenda kuwapongeza wazazi kwa kuwasomesha wanafunzi hawa nanapenda kuwaambia kwamba hawajapoteza kitu kwasababu hakuna urithi mzuri unaoweza kupita elimu hapa duniani,” alisema

Profesa Ndalichako aliwataka wahitimu hao kutumia elimu waliyopata kwa manufaa yao wenyewe na kwa jamii kwani ulimwengu wasasa unahitaji watu wenye ujuzi na wenye upeo wa kisasa wenye uwezo wa kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Alisema kukua kwa kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni kubwa sana hivyo inahitaji watu waendelee kujielelimsisha kwasababu mambo yanaenda yakibadilika siku hadi siku.

“Wahitimu msichoke kujielimisha na wala msidhani mmefika mwisho kwasababu dunia inakwenda kwa kasi sana na unachokijua leo baada ya mwaka au miaka miwili unaweza kukuta kimebadilika kabisa kwa hiyo endeleeni kutafuta maarifa kulingana na mabadiliko yanayojitokeza,” alisema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com