TBS YATOA MAFUNZO  KWA WAUZAJI NA WAAGIZAJI WA VIPURI VYA MAGARI DODOMA

Bw. Benard Abraham, Afisa Kilimo Mkoa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akifungua semina kwa wauzaji, waagizaji na wasambazaji wa vipuri vya magari na wamiliki wa karakana za magari mkoani Dodoma.

*******************

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mafunzo kwa wauzaji, waagizaji na wasambazaji wa Vipuri vya magari pamoja na wamiliki wa karakana za magari katika Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo leo Novemba 22,2022 Jijini Dodoma Afisa Kilimo Mkoa Dodoma Bw. Benard Abraham akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema Serikali imeazimia kwa dhati kuwaunga mkono wafanyabiashara ili kutoa ajira pamoja na kuwezesha ushindani katika masoko ya ndani, kikanda na yakimataifa nje ya Tanzania.

Amesema Mkoa huo ni moja ya mikoa ya kimakakati katika uwekezaji katika juhudi za kuliletea taifa maendeleo ya haraka kulingana na fursa zilizopohasa kwenye sekta ya biashara na ameneo mengine.

"Wafanyabiashara nchini ikiwa ni pamoja na wamiliki wa karakana za kuundia magari wametambulika kuwa sehemu ya washiriki katika kukuza uchumi wa taifa kwasababu wanao mchango mkubwa katika kukuza pato la taifa na kutengeneza ajira kwa wananchi walio wengi". Amesema

Aidha amesema kuwa msukumo wa Serikali kuona kila mmoja anawajibika ili uchumi uendelee kukua na hata kufikia ngazi ya kuwa moja ya nchini zenye uchumi mkubwa duniani.

Pamoja na hayo ameipongeza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa maandalizi mazuri ya warsha hiyo muhimu na ameomba utaratibu wa kufanya warsha kama hizo uwe endelevu ili kuhakikisha wafanyabishara wanakuwa na uelewa sahihi juu ya taratibu mbalimbali katika kuagiza bidhaa zaoili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya kati (TBS), Bw.Nickonia Mwambene amesema mafunzo hayo yamelenga sekta muhimu katika sekta binafsi ambayo inachangia pato la taifa na kuongeza ajira.

Amesema Shirika linaunga mkono mipango na juhui zinazofanywa na serikali ili kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini zinakidhi matakwa ya ubora ikiwemo vipuri vya magari na karakana zinazotumia vipuri hivyo ili biashara iwe inafanywa katika mifumo inayoeleweka.

Amesema kuwa mafunzo hayo pia yamefanyika katika mikoa ya Arusha na Mwanza yakilenga kuwaandaa washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa kiuweledi katika kutekeleza matakwa ya viwango husika pamoja na huduma wanazotoa kwa jamii.

"Hii inatokana na ukweli kwamba sio watu wote wanaweza kushiriki katika sekta hii ya biashara ya vipuri na karakana za magari". Amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post