Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TUTALIPA MSUKUMO SOMO LENYE KOMBINESHENI KIARABU ILI LIFUNDISHWE KIDATO CHA TANO NA SITA : WAZIRI MKENDA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akivalishwa taji na Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Dkt. Musa Salim katika Mahafali ya Shule za Kiislamu za Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika leo Novemba 6,2022 katika uwanja wa Garden jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akiwasili na kupokelewa kwenye viwanja vya Garden jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya Shule za Kiislamu za Ilala Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika leo Novemba 6,2022. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akitunuku vyeti kwa wanafunzi katika Mahafali ya Shule za Kiislamu za Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika leo Novemba 6,2022 katika uwanja wa Garden jijini Dar es Salaam.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika Mahafali ya Shule za Kiislamu za Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika leo Novemba 6,2022 katika uwanja wa Garden jijini Dar es Salaam. Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Dkt. Musa Salim akizungumza katika Mahafali ya Shule za Kiislamu za Ilala Mkoa wa Dar es Salaam,yaliyofanyika leo Novemba 6,2022 katika uwanja wa Garden jijini Dar es Salaam.

****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema atalipa msukumo somo lenye kombinesheni kiarabu ili lifundishwe kidato cha tano na cha sita kwa sababu itasaidia kuzalisha wataalam wataokwenda kukalimani kiarabu na kiswahili kwa kuwa ni lugha kubwa inayotumika umoja wa mataifa.

Ameyasema hayo leo Novemba 6,2022 Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkenda wakati wa Mahafali ya Shule za Kiislamu za Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika katika uwanja wa Garden jijini Dar es Salaam.

Amesema somo la dini lipo kwenye mjadala ikiwamo masuala muhimj ya kuzingatia.

Aidha amesema kuwa jamii haiwezi kukwepa suala la malezi bora kielimu na kimaadili hivyo ni wajibu wa walimu na wenye shule, wana jukumu la kuhakikisha kuwa watoto wanapata malezi ambao wazazi wanataraji ikiwamo kuwapo maadili mema,

"Natoa wito kwa viongozi wa dini kwa kushirikiana na wamiliki wa shule na waalimu wasimamie malezi ya vijana,watumie bidii zote kuhakikisha linakuwa suala la maadili liwe muhimu sana na ninalaani vikali sana wale walioruhusu ule mchezo katika shule ile na mtu kurekodi video". Amesema Waziri Mkenda.

Amesema Serikali inalaani vikali walioruhusu vitendo visivyo vya kimaadili katika shule ya Pwani na inaendelea kufuatilia sakata hilo na itachukua hatua kali kwa kila mwalimu aliyehusika na tukio hilo kwa sababu sio rahisi wanafunzi kufanya vitendo hivyo bila mwalimu yotote kuwa na taarifa.

Ameeleza kuwa suala la maadili liwepo hata katika kusimamia mitihani, kwa kuwa unapowafudisha watoto kuibia mitihani unawafundisha kuwa wezi hapo baadaye.

Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Dkt. Musa Salim, amesema katika uislamu suala la elimu limepewa kipaumbele, kwamba tangu mtu anapozaliwa hadi anapofariki anapaswa kuendelea kujifunza hivyo kuwataka wanafunzi hao kuishika elimu.

"Tunawahusia watoto wetu, tunaowaaga leo na watakaoendelea,kushikamana na maadili, elimu haina maana yote mbele ya jamii iliyokosa maadili, nyinyi ndio taifa la baadaye, nchi hii inawategemea katika suala la madili, endapo taifa litakosa maadili ni sawa na kusema taifa hilo ni mfu". Amesema.

Hata hivyo ameitaka jamii ya kiislamu kujitafakari kwa kuwa ndio inayoongoza kwa mmomonyoko wa maadili, akitolea mfano kuwa kati ya panya road 10, saba ni waislamu,jambo linaloitia aibu serikali na jamii kwa ujumla.

Aidha ameitaka jamii kutoeneza picha au video zinazoonyesha vitendo visivyo na maadili katika mitandao ya kijamii kwa kuwa hiyo inachangia kuporomosha maadili hayo, ametolea mfano video iliyosambazwa ilionyesha wanafunzi wa shule ya mkoani Pwani wakifanya matendo yasiyo na maadili.

Nae Ofisa Elimu Wilaya ya Ilala, lhaji Musa Ally, amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imepokea Sh.bilioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ili kuweka mazingira mazuri ya kufundishia katika Mkoa huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com