Na Dotto Kwilasa,DODOMA.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari na kuongeza kuwa baada ya tukijiridhisha kama hakutakuwa na changamoto ,chama kitaruhusu uchaguzi kufanyika na kama watabaini changamoto wataondosha wagombea wenye changamoto na wasio na changamoto kuendelea na uchaguzi kwa nafasi husika.
Amesema baada ya uchunguzi wa kina wa changamoto katika maeneo husika ,hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wahusika kugombea na kisha kuwakabidhi katika vyombo vyenye dhamana ya kufuatilia masuala ya rushwa.
“Mikoa ambayo tumefanya uamuzi ni pamoja na kufuta uchaguzi wa umoja wa Vijana mkoa wa Simiyu , pia tumesimamisha uchaguzi wa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mbeya kwa sababu ya tuhuma mbalimbali zikiwemo za rushwa ambako nako tunafanya uchunguzi wa kina tukikamilisha tutatoa taarifa ya uamuzi wa chama,"amesema Chongolo.
Pamoja na hayo amesema," tumesimamisha uchaguzi wa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Arusha kwa sababu hiyo hiyo ya rushwa na tukikamilisha uchunguzi tutatoa taarifa za uamuzi wa chama ili kuruhusu mchakato wa uchaguzi kuendelea".
Katibu Mkuu huyo pia amezungumzia kuhusu tukio la wanachama kuondoka na boksi la kura katika uchaguzi uliofanywa jana (juzi) mkoa wa kichama wa Magharibi Zanzibar na kueleza kuwa watu hao walienda na boksi hilo kwenye chumba kilichokuwa kimeandaliwa kwa ajili ya kuhesabia kura .
“Sasa tunataka kuangalia uchukuaji wa boksi hilo ulilenga kuhesabu kura au ulikuwa una lengo lingine,tutafuatilia tukijiridhisha tutachukua uamuzi ukiwemo kuufuta uchaguzi na kurudiwa upya ili kutenda haki ,tukijiridhsisha kwamba lengo la kuchukua boksi hilo ulilenga kwenda kuhesabu kura basi tutaruhusu matokeo ya uchaguzi huo yaendelee kama yalivyo.”amesema
Aidha Chongolo amezungumzia kuhusu changamoto iliyopo sasa ndani ya chama hicho kuwa ni kuwepo kwa wajanja wachache wanaogombea nafasi mbalimbali au wapambe wao kutengeneza msukumo wa kuonyesha wao ni maalum kuliko wengine na wao ndio wanaotakiwa na viongozi wa juu kuliko wengine.
“Wapo humu wengine wanajiita wagombea wa katibu Mkuu ,wapo wanaojiita wagombea wa Makamu Mwenyekiti ,wengine wanajiita wagombea wa Mwenyekiti na wapo wanaojiita wagomeba wa wajumbe wa kamati kuu,sisi tulishapitisha majina,na kama tumepitisha kwenye mkoa majina matatu ,moja ,mawili au manne na kuendelea maana yake hao ndiyo wagombea wa chama,"amesema.
Social Plugin