Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa,(OR-Tamisemi) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART uliofanyika leo Novemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam Mwanyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara, Dkt. Florens Turuka akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART uliofanyika leo Novemba 15,2022 Jijini Dar es SalaamMtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART, Dkt. Edwin Mhede akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART uliofanyika leo Novemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa,(OR-Tamisemi) Mhe. Angellah Kairuki akikabidhi vitendeakazi kwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo Novemba 15,2022 Jijini Dar es SalaamWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa,(OR-Tamisemi) Mhe. Angellah Kairuki akipata picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo Novemba 15,2022 Jijini Dar es SalaamWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa,(OR-Tamisemi) Mhe. Angellah Kairuki akipata picha ya pamoja na wadau wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART uliofanyika leo Novemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa,(OR-Tamisemi) Mhe. Angellah Kairuki ameitaka Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART kuhakikisha inafanya kazi kwa bidii katika kubuni mikakati ya kuboresha zaidi huduma ya usafiri ndani ya Jiji la Dar es Salaam na ikiwezekana kuchukua hatua za kuanzisha huduma hiyo katika majiji mengine nchini.
Wito huo ameutoa leo Novemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART na kusema uanzishaji wa chombo hicho cha Serikali chini ya usimamizi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ni muhimu kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya nchi kijamii na kiuchumi.
Aidha, amesema chombo hicho kina wajibu wa kuhakikisha kinasimamia utekelezaji na uendeshaji wa Mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka katika Jiji la Dar es salaam ili azma ya Serikali katika uanzishaji wake iweze kutimia.
Amesema kutokana na usimamizi imara unaofanywa na DART chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI katika kutekeleza mradi wa DART, Jiji la Dar es Salaam limefanya uamuzi thabiti wa kutoa huduma hii ya usafiri katika ubora wa kiwango cha kimataifa.
"TAMISEMI inaendelea na hatua za utunzi wa Sheria ya Usafiri wa Umma Mijini ambapo pamoja na mambo mengine, kupitia Sheria hiyo inapendekezwa kuanzisha chombo chenye mamlaka ya kutekeleza majukumu yake kihuduma, kibiashara (kwa kushirikiana na sekta binafsi) na kwa uharaka zaidi katika kuwafikia wananchi kwa huduma ya usafiri wa umma na kuondokana na utegemezi wa ruzuku ya Serikali". Amesema Waziri Kairuki.
Pamoja na hayo amesema kutokana na kazi zinzoendelea katika ujenzi wa miundombinu Awamu ya Pili kwa barabara iendayo Mbagala Rangitatu, na huduma ya mabasi inayoendelea Awamu ya Kwanza katika Barabara ya Morogoro na maeneo mengine kama vile Hospitali ya Mloganzila na Kibaha (Mkoa wa Pwani) , ni dhahiri kuwa DART, inatakiwa kujipanga kupambana na changamoto za usafiri wa umma zitakazoongezeka katika jiji la Dar es Salaam.
Amesema ongezeko la idadi ya watu katika Jiji la Dar es Salaam kwa mwongo uliopita limekuwa kubwa zaidi kuliko kasi ya uboreshaji wa miundombinu na hivyo kwa kiwango kikubwa kuongeza msongamano wa magari barabarani. Jiji la Dar es Salaam.
Nae Mwanyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara, Dkt. Florens Turuka amesema Bodi itahakikisha inakuwa bega kwa bega na uongozi wa menejimenti ya Wakala kusaidia utekelezaji wa mikakati ya utekelezwaji wa program zote zilizopo na zinazoendelea ili zikamilike kwa wakati.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART, Dkt. Edwin Mhede amesema Ujenzi wa miundombinu ya awamu ya pili ya Mradi wa DART unatekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 141.71.
Amesema Serikali imelipa fidia ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 30.25 kwa wananchi wapatao 92 ambao maeneo yao yaliathiriwa na utekelezaji wa mradi huu katika mitaa ya Mianzini (Mbagala), kwa Azizi Ally, Misheni na Chang’ombe.
Pamoja na hayo amesema Wakala unaendelea kukamilisha zabuni ya kununua mabasi 177 ili kuweza kukamilisha idadi ya mabasi 387 kulingana na usanifu, ili kukamilisha awamu ya kwanza kuweza kutoa huduma kamili kikamilifu.
Social Plugin