*********************
NA EMMANUEL MBATILO
FISTON Kalala Mayele amendelea kutikisa nyavu ndani ya ligi kuu NBC baada ya leo kupachika mbao mawili na kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi wa mabao mawili dhidi ya Dodoma Jiji.
Mchezo huo ambao ulichezwa kwenye dimba la Liti mkoani Singida tumeshuhudia wachezaji wengi wa Yanga kupata majeruhi kwenye mchezo huo akiwemo nahodha wao Bakari Nondo Mamnyeto na Feisal Salum.
Kipindi cha kwanza Yanga Sc ilikuwa mbele kwa bao 1-0, bao ambalo lilifungwa kabla ya kwenda mapumziko dakika ya 43 ya mchezo.
Social Plugin