VRB YATOA MAFUNZO YA USAJILI WA KUDUMU KWA WATHAMINI 121 NCHINI 

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wathamini (VRB), FRV.Dkt.Cletus Ndjovu akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya usajili wa kudumu wa wathamini ambayo yamefunguliwa leo Novemba 1,2022 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wathamini (VRB), FRV. Joseph Shewiyo akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya usajili wa kudumu wa wathamini ambayo yamefunguliwa leo Novemba 1,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi FRV.Dkt.Upendo Matotola akitoa mafunzo kwa wathamini katika Mafunzo ya usajili wa kudumu wa wathamini ambayo yamefunguliwa leo Novemba 1,2022 Jijini Dar es Salaam. Sehemu ya Wathamini wakiwa kwenye Mafunzo ya usajili wa kudumu wa wathamini ambayo yamefunguliwa leo Novemba 1,2022 Jijini Dar es Salaam.

**********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BODI ya Usajili wa Wathamini Tanzania (VRB) wameendesha Mafunzo ya usajili wa kudumu wa wathamini 121 ambao wataenda kunufaika na usajili wa kudumu na kuweza kupata fursa ya kujitegemea katika kujiajiri.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo Mthamini kutoka Bodi ya Usajili wa Wathamini Tanzania (VRB), FRV Christopher Kilatu amesema Mafunzo hiyo ni ya wiki tatu darasani ambapo wanafunzi watajifunza kozi mbalimbali ambazo zitaweza kuwafanya waweze kufaulu na kuweza kupata usajili wa kudumu.

"Wakishajifunza darasani kutakuwa na zoezi la wanafunzi kwenda kufanya uthamini kwa vitendo na baadae watafanya mawasilisho (presentation) ya hizo kazi zao na watakaofaulu watakuwa wamehitimu mafunzo yao ya usajili wa kudumu na kupewa vyeti". Amesema FRV Kilatu

Amesema Mafunzo hayo ni ya wathamini ambao tayari wameshasajiliwa na bodi na wanataka kuhama kutoka usajili wa awali kwenda kwenye usajili wa kudumu.

Aidha amesema Mafunzo hayo yanakwenda kupanua wigo kwa wathamini katika kufanya kazi zao, kwasababu kisheria wathamini wakiwa katika usajili wa ngazi za awali hawawezi kufanya kazi wao wenyewe mpaka wasimamiwe. 

"Hawa wanaosoma haya mafunzo sasa hivi wakishahitimu na kufaulu watapata usajili wa kudumu hivyo wanaweza kwenda kufanya kazi wao wenyewe na kuwapa fursa ya kuweza kufungua kampuni na kusimamia kazi mbalimbali, amesema Kitalu"

Kwa upande wake Glory Tesha ambaye ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo amesema watanufaika kwa ujuzi ambao watapatiwa na vilevile wataweza kujiajiri kwani wathamini mara nyingi sokoni wanakuwa na ushindani hasa makampuni ambayo mwanzoni yalikuwa ni machache lakini kwa sasa mafunzo hayo ni njia nzuri kwa wathamini wadogo kuweza kujiajiri.

Nae Mshiriki mwingine wa mafunzo hayo PRV Petro Michael amesema kupitia mafunzo hayo watapata ujuzi ambao utawasaidia kulitumikia taifa kwa ujumla kwani idadi ya wathamini wanaoshiriki katika mafunzo hayo ni kubwa na matumaini yao ni kuona wote wanafaulu na kupatiwa vyeti.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post