Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AIRTEL YAZINDUA KUWA MJANJA TUMIA AIRTEL MONEY, TUMA PESA BILA TOZO MSIMU WA SIKUKUU

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano akifafanua jambo akiwa ameshikilia bango la uzinduzi wa Kuwa Mjanja Tumia Airtel money  ambapo kampeni hiyo itawazesha wateja kutuma pesa hadi milioni 5 bila kulipia TOZO kwa miamala yote wanayofanya kupitia Applikesheni ya Airtel katika msimu huu wa sikukuu. Kulia ni Meneja wa Chapa wa Airtel Money Bi Gillian Rugumamu.

**
  • Tuma pesa na Airtel Money gharama za TOZO zimelipwa na Airtel kwa miamala ya hadi 29,9999 muda wowote na mahali popote
  • Tuma hadi Milioni 5 bila gharama ya Tozo -Kuwa mjanja hii ni ukitumia Aplikesheni ya Airtel Kufanya Muamala
  • Airtel Money Wakala wameenea nchi nzima Zaidi ya wakala 160,000 na Maduka ya Airtel Money Branch 3,500 wako Kila kona kukuhudumia.

Dar es Salaam Jumanne 6 Disemba 2022 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzaia kupitia huduma ya Airtel Money leo imetangaza kuzindua kampeni yake mpya ya Kuwa Mjanja tumia Airtel Money inayolenga kuongeza unafuu zaidi kwa wateja wetu wote wanaotumia huduma ya Airtel Money kwa kulipia huduma mbali mbali kwa kujinufaisha binafsi na kuinua uchumi wa taifa kupitia huduma za fedha kidigitali.

Uzinduzi wa kampeni  ya na hivyo kumfanya mteja wa Airtel Money kupata unafuu Zaidi pale wanapofanya miamala popote.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampeni hiyo ya Kuwa Mjanja tumia Airtel Money, Mkurugenzi wa mawasiliano Airtel Bi, Beatrice Singano alisema kuwa “Kampeni hii ni muendelezo wa upendo wetu kwa wateja wote wanaotumia Airtel Money.

“Kuwa Mjanja tumia Airtel Money inakuja baada ya hivi karibuni Airtel kuwepo kwa OFA  kabambe ya Airtel Money Bila Tozo Ofa ambayo inampa mteja wa Airtel Money unafuu wa kutuma au kutoa fedha bila tozo.

“Airtel tunafahamu   msimu huu tunaokwenda kwenye sikukuu nyingi za mwisho wa mwaka wengi tunahitaji kutuma, kutoa au kupokea pesa mikoani, tumia Airtel Money ni nafuu kwa kuwa hakuna tozo,  gharama za tozo zimelipwa na Airtel kwa miamala ya hadi 29,9999 na unaweza kuitumia Airtel Money muda wowote na mahali popote”.alieleza Bi Singano

Pia ukitumia App ya Airtel kutuma pesa hadi milioni tano ni BURE yaani hakuna TOZO yoyote serikali inayolipwa na mteja. Airtel italipa tozo kwa nia ya mteja

“Airtel Money ndio huduma ya kifedha kwa njia ya simu za mkononi ambayo pia wateja wa wanaweza kujipatia mkopo rahisi ili kukamilisha miamala yao kupitia huduma ya mikopo ya Kamilisha wakiwa popote. Bi Singano alisisitiza ‘Kuwa Mjanja Tumia Airtel Money kamilisha miamala yako kwa uhuru bila kusambaza usiri wa jambo lako ukiwa popote muda wowote”.

Airtel Money imekuwa ikija na bidhaa na huduma nafuu, salama, na uhakika  wakati wowote za ambazo zinaendana na mtindo wa maisha ya sasa kwa wateja wetu.

 

Huduma za Airtel Money zinakuwezesha kupunguza gharama zisizo na ulazima kwa kurahishisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa mtu binafsi au hata biashara. Kwa mtu anayepokea fedha kutoka nje ya nchi kwa sasa haitaji tena kusafiri umbali mrefu ili aweza kupata fedha zake. Airtel Money imeshafungua maduka ya Airtel Money branches zaidi ya 3,500, mawakala zaidi ya 160,000 ili kutoa huduma mbalimbali za Airtel kila kona ya nchi.

 

Airtel imefanya uwekezaji mkubwa na Airtel Money kuunganishwa na makampuni zaidi ya 1,000 ya watoa huduma mbali mbali,

 

Vile vile Airtel Money imeunganisha zaidi ya taasisi 40 za kifedha kuwahudumia wateja wa benki na hata wasio wa benki hizo.

 

Airtel Tanzania bado inandelea na dhamira yake ya kupanua huduma zake kote nchini kwa kasi ili kuendelea kutoa suluhisho mbalimbali kutokana na uhitaji wa wateja wote.

Mkurugenzi wa mawasiliano Airtel Bi, Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari leo wakati wa akizindua kampeni ya Kuwa Mjanja tumia Airtel Money  inayoendeleza unafuu zaidi kwa wateja wa Airtel Money ikiwemo ofa ya kutuma pesa kwa Airtel Money Bila gharama za TOZO kwa miamala ya hadi 29,999 muda wowote na mahali popote. Kulia ni Meneja wa Chapa wa Airtel Money Bi Gillian Rugumamu
Mkurugenzi wa mawasiliano Airtel Bi, Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari leo wakati wa akizindua kampeni ya Kuwa Mjanja tumia Airtel Money  inayoendeleza unafuu zaidi kwa wateja wa Airtel Money ikiwemo ofa ya kutuma pesa kwa Airtel Money Bila gharama za TOZO kwa miamala ya hadi 29,999 muda wowote na mahali popote. Kulia ni Meneja wa Chapa wa Airtel Money Bi Gillian Rugumamu
Mkurugenzi wa mawasiliano Airtel Bi, Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari leo wakati wa akizindua kampeni ya Kuwa Mjanja tumia Airtel Money  inayoendeleza unafuu zaidi kwa wateja wa Airtel Money ikiwemo ofa ya kutuma pesa kwa Airtel Money Bila gharama za TOZO kwa miamala ya hadi 29,999 muda wowote na mahali popote. Kulia ni Meneja wa Chapa wa Airtel Money Bi Gillian Rugumamu 
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano akifafanua jambo akiwa ameshikilia bango la uzinduzi wa Kuwa Mjanja Tumia Airtel money  ambapo kampeni hiyo itawazesha wateja kutuma pesa hadi milioni 5 bila kulipia TOZO kwa miamala yote wanayofanya kupitia Applikesheni ya Airtel katika msimu huu wa sikukuu. Kulia ni Meneja wa Chapa wa Airtel Mopney Bi Gillian Rugumamu. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com