Uchunguzi wa awali kuhusu ajali iliyoondoa uhai wa wanandoa Tumaini John na Geofrey John mkoani Kagera unaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva mmoja wa pikipiki aliyekuwa amepakia magunia ya mkaa kuisukuma pikipiki waliyokuwa wamepanda watu hao.
Aidha majirani wa wanandoa hao wameeleza kuwa wakati wanapata ajali hiyo mume alikuwa akimpeleka mke wake kazini kwa kutumia pikipiki baada ya gari lao kupata pancha.
"Waliofariki ni mume na mke, wameacha watoto watatu mkubwa wa kiume yupo kidato cha tatu na wa mwisho bado ni mdogo zaidi ananyonya", amesema Joachim Kahumbi ambaye ni jirani wa wanandoa hao.
Chanzo - EATV
Social Plugin