Mkurugenzi wa Benki ya CRDB nchini Congo, Jesca Nachiro (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Plasduce Mbossa wakiwa wameshika banngo lenye kutambulisha mfumo mpya wa malipo ya kadi kwa wateja wa Bandari uliorahisishwa kupitia Benki ya CRDB, katika hafla ya uzinduzi huo huo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Bandari, jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha na Uondoshaji Shehena Bandarini, Edward Urio akishuhudia pamoja na wadau wengine.
Wakati Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ikizindua mfumo wa Malipo kwa njia ya ya kidijitali jijini Dar Es Salaam Desemba 30, 2022, imeelezwa kuwa sehemu kubwa ya uanzishwaji wa mfumo huo imefanikishwa na Benki ya CRDB ambayo imekuwa kinara wa mifumo ya malipo hapa nchini kwa miaka mingi.
Akizungumza kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Nchini Congo, Jesca Nachiro amesema uzoefu mkubwa ambao benki hiyo unao katika katika mifumo ya malipo ndio iliyopelekea kuishauri Mamlaka ya Bandari kuanzisha kwa mfumo huo ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato lakini na kurahisha huduma za malipo kwa wadau.
Nyachiro ameishukuru Mamlaka hiyo kwa kuichagua Benki ya CRDB kuwa mshiriki katika utengenezwaji wa mfumo huo utakao wawezesha wateja wa bandari kufanya malipo popote walipo.
“Tunajivunijia kuona Benki yetu imeshiriki kwa kiasi kikubwa kuanzisha mfumo huu, tukiwa Benki ya kwanza kuunganisha huduma setu na mfumo. Ni imani yetu kuwa mfumo huu uleta mapinduzi makubwa kwa kuwezesha wateja wa Bandari kufanya malipo duniani kote,” alisema.
Akizungumzia kuhusu mfumo huo Nyachiro amesema kuwa utaenda kufunga mianya yote ya udanganyifu ambayo wateja walikuwa wakilalamikia kwa kupewa kiwango cha malipo kisicho sahihi.
Aliongezea kuwa Mfumo huo utaleta mapinduzi kwa TPA kwani pia unabadilisha fedha za kigeni bila mtu yeyote kuhusika.
Aidha alisema kwa kuzingatia kuwa TPA inahudumia nchi nyingi hivyo mfumo huo utawarahisishia kupata huduma kwa urahisi kwakufanya malipo kwa urahisi zaidi, ambapo malipo yatafanyika popote mteja alipo bila kulazimika kwenda benki.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa amesema kuwa mfumo huo utaenda kurahisisha utendaji wa bandari kwani ulipaji wa kutumia 'Control number' utatumika katika ufanyaji malipo yote ya bandari.
Amesema kuwa mfumo huo utasoma kila hatua ya malipo yanayofanyika kwa wateja katika kulipia malipo mbalimbali ambayo yatakuwa yamefanyika.
Mbossa aliishukuru Benki ya CRDB kwa kushiriki mchakato mzima wa uanzishwaji wa mfumo huo ambao pia umeunganishwa na mifumo ya kimataifa ya malipo ya Visa na MasterCard. Alibainisha kuwa VISA na Master Card ni mhimu katika biashara zinazofanyika kimataifa kwani zinatambulika kimataifa hivyo mfumo huo utarahishisha hata utendaji kazi wa Mamlaka kwa Ujumla.
Pia amesema mfumo huo utapunguza urasimu na foleni ambazo zilikuwa zinajitokeza hapo awali, pia amesema kuwa TPA itafungua kituo kikubwa cha huduma kwa wateja ili kuweza kutoa huduma kwa wateja pale wanapopata changamoto mbalimbali za Kiteknolojia wakati wa kufanya malipo.
Akizungumza wakati anazindua mfumo huo Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha na Uondoshaji Shehena Bandarini, Edward Urio aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali katika nyanja mbalimbali hususani katika kuleta mapinduzi ya kidigitali kwakurahisisha ukusanyaji wa mapato nchini. Aliipongeza Benki hiyo kuweza kubuni na kukamilisha mfumo ambao utakwenda kuleta mapinduzi makubwa na hivyo kuongeza ukusanyaji wa mapato katika Bandari zetu.
“Mfumo huu ni mahususi katika kusaidia ulipaji wa huduma zitolewazo na mamlaka ya bandari kwa wateja mbalimbli wa ndani na wa nje kutoka nchi nufaika zinazo pata huduma katika mamlaka ya badari nchini,” alisema.
Taasisi mbalimbali za kifedha zikiongozwa na Benki ya CRDB zimeunganisha mifumo yao ya malipo katika mfumo huo jambo ambalo linatarajiwa kuwawezesha Watanzania wengi wanaaotumia bandari hiyo kufanya malipo kwa urahisi.
Social Plugin