Huenda isiwe taarifa nzuri kwa mashabiki wa Yanga, lakini ndivyo ilivyo inadaiwa kuwa, kiungo fundi wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ anajiandaa kuondoka klabuni hapo.
Kiungo huyo aliyesajiliwa misimu minne iliyopita kutoka JKU ya Zanzibar, inaelezwa ameamua kuvunja mkataba na klabu hiyo ili awe huru kujiunga na timu yoyote kupitia dirisha dogo la usajili lililopo wazi hadi Januari 15 mwakani.
Tangu mapema, Fei mwenye mabao sita katika Ligi Kuu Bara msimu huu na asisti mbili, amekuwa akihusishwa na klabu ya Azam, ila pande zote ikiwamo mchezaji mwenyewe, wamekuwa wakikanusha juu ya kuwepo kwa dili hilo.
Hata hivyo, chanzo cha kuaminika kilicho karibu na kiungo huyo kimesema, Fei ameamua kujichomoa klabuni hapo kutokana na kutotekelezwa kwa ishu yake ya kimasilahi ikiwamo ombi la ongezeko la mshahara anaolipwa Yanga.
ENDELEA KUSOMA <<HAPA>>
CHANZO - MWANASPOTI
Social Plugin