Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI GWAJIMA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA ASKOFU SANGU...APONGEZA KANISA KWA SERA ZINAZOGUSA FAMILIA NA USTAWI WA JAMII

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiagana na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu alipokutana naye leo Jumatatu Desemba 5,2022 katika makazi ya Askofu yaliyopo Kanisa kuu Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga na kufanya mazungumzo mafupi kuhusu nafasi ya Kanisa, katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu alipokutana naye leo Jumatatu Desemba 5,2022 katika makazi ya Askofu yaliyopo Kanisa Kuu Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga na kufanya mazungumzo mafupi kuhusu nafasi ya Kanisa katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akipiga picha na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu alipokutana naye leo Jumatatu Desemba 5,2022 katika makazi ya Askofu yaliyopo Kanisa Kuu Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga na kufanya mazungumzo mafupi kuhusu nafasi ya Kanisa katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu (kushoto) akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu (kushoto) akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima (kulia)
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu (kushoto) akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja na Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanisa, wa kwanza kushoto ni Katibu wa Askofu Padre Deusdedith Kisumo, wa pili ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi, anayefuata kutoka kwa Waziri Gwajima ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mheshhimiwa Elius Masumbuko , mwenye shati la Bluu ni Mkurugenzi wa masuala ya Fedha jimboni Padre Paschal Kasase na mwenye suti ni Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Donald Tumbo
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiagana na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu alipokutana naye leo Jumatatu Desemba 5,2022 katika makazi ya Askofu yaliyopo Kanisa kuu Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga na kufanya mazungumzo mafupi kuhusu nafasi ya Kanisa, katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

****

Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amemhakikishia Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum Dkt.Doroth Gwajima kuwa, Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga liko pamoja na Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, katika kuunga mkono juhudi za mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Askofu Sangu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Waziri Dkt. Gwajima, ambaye alitembelea katika makazi ya Askofu yaliyopo Kanisa kuu Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga, na kufanya naye mazungumzo mafupi kuhusu nafasi ya Kanisa, katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Askofu Sangu amemuahidi Waziri Gwajima kuendelea kuyasemea mambo yote yanayochangia vitendo vya ukatili katika jamii, ikiwemo mila ambazo zinachochea kuendelea kwa vitendo hivyo na kwamba, Kanisa linayachukulia mapambano dhidi ya ukatili huo kama ajenda yake ya dharura na ya kudumu.

SAUTI YA ASKOFU SANGU

Kwa upande wake Dkt.Gwajima amelipongeza Kanisa Katoliki kwa kuendelea kuunga mkono mipango mbalimbali ya Serikali, na hasa kwa kuweka  sera nzuri zinazogusa masuala ya familia na ustawi wa jamii .

SAUTI YA WAZIRI DKT.GWAJIMA

Dkt.Gwajima ametumia nafasi hiyo  kuzipongeza taasisi zote za dini zinazounga mkono juhudi za serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Ameahidi kutoa ushirikiano kwa taasisi yoyote ya dini kwenye mipango yote inayolenga kuunga mkono juhudi za serikali, katika kukabiliana na mambo mbalimbali yanayokwamisha ustawi wa jamii, ikiwemo vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Leo Jumatatu tarehe 05.12.2022, Waziri Gwajima amekabidhi cheti cha pongezi kwa Redio Faraja inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga, ambacho kimetolewa na wizara yake baada ya kuridhishwa na mchango inaoutoa katika kusaidia mpango wa taifa wa MTAKUWWA, wenye lengo la kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto.

Waziri Gwajima ametumia nafasi hiyo kueleza mkakati mpya wa serikali, ambao umelenga kuwaingiza rasmi Waandishi wa Habari na vyombo vya habari katika mpango wa kuimarisha mifumo ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com