Dereva wa Thailand anadhihakiwa mtandaoni baada ya kumsahau mkewe kwa bahati mbaya aliposimama kujisaidia siku ya Krismasi, na kumlazimu kutembea kwa zaidi ya maili 12 ili kupata usaidizi.
Tukio hilo lilitokea baada ya Boontom Chaimoon, 55 na mkewe, Amnuay Chaimoon, 49, kufunga safari saa tatu asubuhi siku ya Jumapili kwenda kusherehekea Mwaka Mpya katika mji wake ulioko Mkoa wa Maha Sarakham nchini Thailand.
Kulingana na New York Post, kila kitu kilikuwa kikienda sawa hadi mumewe aliposema kwamba alihitaji kujisaida na kuegesha gari lake kando ya barabara.
Inasemekana kwamba Amnuay alimuuliza mahabubA wake kwa nini hakusimama kwenye kituo cha mafuta - lakini alipokosa kujibu, aliamua pia kujisaidia msituni.
Hata hivyo inaonekana kuwa mumewe aliporejea hakugundua mkewe alikuwa ameondoka ndani ya gari kwenda kujisaidia pia. Wakati mama aliporudi alishtuka kupata mumewe ameondoka huku akibaki hoi kichakani giza nalo likianza kuingia.
Akihisi kupotea na kuogopa, Amnuay aliamua kutembea hadi wilaya ya Kabin Buri, iliyoko kilomita 20 (umbali wa maili 12.4).
Baada ya safari iliyoonekana kutokuwa na mwisho, hatimaye alifika katika kituo kimoja cha polisi majira ya saa kumi na moja asubuhi.
Mama huyo alikuwa ameiacha simu yake kwenye begi ndani ya gari hivyo basi ikiwalazimu polisi kumpigia mumewe lakini hakupokea kwa dakika ishirini.
Maafia hao waliamua kuwasiliana na jamaa zake badala ya mwanaume.
Amnuay alihofia kwamba ikiwa hangeweza kumpata mume wake au familia, ingemlazimu kuuza mkufu wake wa dhahabu ili apate hela za usafiri.
Ni hadi saa mbili asubuhi polisi hao walifanikiwa kumpata mwanaume huyo aliyeonekena wazi kuchanganyikiwa ambaye wakatgi huo alikuwa ameendesha gari hadi mkoa wa Korat kilomita 159.6 (karibu maili 100).
Aliposikia alichokifanya, Bontoom aligeuka haraka na kurudisha gari lake hadi Kabin Buri na kumchukua mkewe.
Alipoulizwa ni kwa jinsi gani aliendesha gari hadi bila kutambua kutokuwepo kwa kwa mkewe, jamaa huyo aliyefedheheshwa alisema alifikiri alikuwa kwenye kiti cha nyuma akilala muda wote.
Jamaa alimwomba mkewe radhi.
Licha ya kitendo chake cha kiajabu, Amnuay alisema hawakubishana.
Baadaye alifichua kwamba walikuwa wameoana kwa miaka 27 na walikuwa na mtoto wa kiume wa miaka 26.
Social Plugin