Mzee mwenye umri wa miaka 78 ameumia moyoni baada ya kugundua kuwa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 49 si wake kibayolojia na sasa anadai mahari aliyomlipia mkewe.
Wilson Shirichena kutoka Mhondoro nchini Zimbabwe ambaye aliamini kuwa Milton Shirichena alikuwa mwanawe wa kumzaa kwa miongo minne iliyopita, bado yuko katika mshtuko kufuatia ugunduzi huo wa kushangaza.
Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba Wilson alidai kwamba Milton alidhaniwa kuwa “mwanawe” alitembelewa na babake halisi, ambaye alimwambia kwamba alikuwa mwanawe kabla hajafa.
Kwa maneno yake alisema; “Nilipoambiwa hivyo, niliumia sana moyoni kujua kwamba mke wangu mpendwa angenificha kwa miaka 43. Sasa nadai nilipwe pesa zangu za mahari kutoka kwa Milton kwa vile nililipa uharibifu ambao ulipaswa kulipwa na baba yake mzazi, ambaye alimpa mimba mke wangu kabla hatujaoana.
“Mke wangu hajisikii vizuri. Ana matatizo ya akili, na wakwe zangu wote walikufa. Kwa hiyo Milton anapaswa kunilipa pesa zangu badala ya baba yake.”
Milton hata hivyo alikanusha madai kwamba alizungumza na anayedaiwa kuwa "baba yake mzazi" alipokuwa bado hai.
Alisema; “Siwezi kukataa kwamba kuna maneno yanaenea kuwa mimi si mtoto wa Wilson, lakini hatujawahi kuzungumzia jambo hilo, ikiwa ana uthibitisho wa anachokisema basi afuate taratibu zinazopaswa kufanywa kuliko kukimbizana na mimi kutoka kwa familia kama mbwa."
Via Tuko News
Social Plugin