Wakiwa wamesimama kwenye madhabahu kwa ajili ya harusi yao ya kanisani, bwana harusi ghafla alimpiga bibi harusi wake kofi usoni.
Tukio hilo lisiloelezeka ambalo halijajulikana limetokea wapi limenaswa katika video iliyoshirikiwa na @esthernice2 kwenye TikTok.
Kabla ya kofi hilo, bwana harusi alionekana kumsogelea mke wake kana kwamba anataka kumpiga busu. Lakini hatimaye hakumbusu na akakubali kumpiga kofi.
Haijabainika ni nini huenda kilichochea hatua yake kwani sauti ya video hiyo haikueleweka na klipu hiyo haikuzidi sekunde 17.
Kioja hicho kilizua hisia mesto miongoni mwa watu.
Social Plugin