Nabii Mkuu wa kanisa la Ngurumo ya Upako ambaye pia ni balozi wa Amani Afrika Dkt. Geordavie Kasambale ameahidi kuwaunga mkono wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la Samunge (NMC) waliopata janga la kuunguliwa na soko mwaka 2020 kwa kuwagawia fedha za mitaji pamoja na kuwatengenezea baadhi ya miundombinu ya soko.
Akiongea katika ibada iliyofanyika katika kanisa Ngurumo ya upako alisema kuwa anatarajia kwenda kuwapa misaada ya mitaji pamoja na vitu vingine vya sokoni Desemba 30 mwaka huu.
"Nilipokea barua kutoka Kwa wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) wa soko la Samunge wakiwa wanataka msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo mitaji ,miundombinu ya soko napenda kuwaambia nimekubali na mwezi huu tarehe 30 nitaenda sokoni hapo Kwa ajili ya kuwasaidia", alisema nabii Mkuu Dkt GeorDavie
Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa soko la Samunge (NMC)Mraji Njola alisema kuwa wao kama wafanyabiashara wadogo walikaa chini na kuamua kumuandikia barua nabii mkuu Dr. GeorDavie ya kumuomba msaada wa miundombinu ya soko ikiwemo mageti ,mitaro pamoja na mitaji .
"Mwaka 2020 tuliunguliwa na soko hili la Kilombero na wafanyabiashara wengi walipoteza mitaji yao na hata sisi unavyotuona tumeanza upya na hatuna mitaji hivyo tukaona tumtumie nabii barua ya kuomba msaada na tunashukuru Mungu amekubali na ametuhaidi kuja kutuunga mkono Desemba 30 mwaka huu tumefurahi sana na tunamsubiri kwa hamu",alisema
Alisema kuwa soko lao lina ukosefu wa miundombinu kama mageti ambayo iwapo yatawekwa itasaidia kupunguza wizi unaotokea mara kwa mara katika soko hilo,pia kutengenezwa mitaro ya maji itapunguza tatizo la maji kujaa katika soko haswa katika kipindi cha mvua .
"Katika soko hili kuna wanawake wengi ambao ni wajane wanaotegemea kufanya biashara kwenye soko hilo waweze kulea familia zao na wengi wao walipoteza mitaji kipindi kile ambacho soko liliungua hivyo ujio wa kiongozi huyu wa dini itatusaidia kurudisha tumaini jipya na ndoto zetu ambazo tulikuwa nazo kabla ya kuunguliwa kwa soko"alibainisha
Aidha aliwataka viongozi wengine wa madhehebu mengine ya dini kuiga mfano wa nabii Mkuu wa kusaidia jamii haswa zile za maisha duni ili kuweza kusaidia serikali kuwaondoa watu kwenye umaskini.
"Unajua nabii Mkuu amekuwa ni kiongozi wa dini ambaye anasaidia sana jamii ukiangalia amesaidia vijana kuna aliowapa pikipiki,Kuna aliowapa bajaji ,kunawanawake wamepewa mitaji ,kunaanao walipia wanafunzi ada hii yote ni kuhakikisha anawatoa watu katika kujikwamua kwenye umaskini tukipata viongozi wa dini wengine kama huyu kwakweli watasaidia sana kuosaidia serikali kutoa ajira na kupambana na umaskini "alisema Mwaji Daudi (Mama Shilooo) mfanyabiashara mdogo wa soko la Samunge
Naye mfanya biashara mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Mangenyi aliitaka serikali kuendelea kuwaunga mkono viongozi wa dini ambao wanasaidia jamii kujikwamua katika umaskini.
Social Plugin