Huko Ohio, Marekani, mwaka 2016 Polisi waliripoti wametumiwa picha na mhalifu waliyekuwa wanamtafuta.
Jamaa anaitwa Donald Pugh (pichani), aliwatumia picha Polisi na kuwaomba wabadilishe picha waliyokuwa wameweka kwenye bango la tangazo la kutafutwa kwake kwa sababu ilikuwa inaonekana vibaya, hivyo aliwatumia picha hiyo nzuri ili watu wasimuone kama ana sura mbaya.
Polisi walikubali ombi lake wakaweka picha aliyokuwa anataka na pia wakamshukuru kwa ushirikiano alioonesha na kumuomba kama ikiwezekana aende kituo cha Polisi wazungumze.
Social Plugin