Mwigizaji maarufu wa vichekesho wa kipindi cha "Vioja Mahakamani" kinachorushwa na runinga ya KBC cha Kenya Gibson Gathu Mbugua, almaarufu 'Kiongozi wa Mashtaka', amefariki dunia.
Familia ya Gibson imeeleza kuwa mchekeshaji huyo amefariki dunia leo Alhamisi, Desemba 22 akiwa katika Hospitali ya Mediheal
"Habari za asubuhi marafiki na familia... Asubuhi ya leo nimepigiwa simu kutoka Hospitali ya Mediheal ikinijulisha kuwa ndugu yetu Gibson amepumzika. Imekuwa safari lakini kwa yote Mungu bado yuko kwenye kiti cha enzi," ulisomeka ujumbe huo kutoka kwa familia hiyo.
Gibson Mbugua ametajwa kuwa ugonjwa wa kisukari kwa zaidi ya miaka 20 na baadae alipata shida kwenye figo yake mnamo Novemba 2020 iliyomfanya aandae harambee ya kumchangia gharama za upasuaji wa figo. Bw. Mbugua alilazwa hospitalini mnamo mwezi Julai baada ya michango ya wasamaria wema ya pesa za Kenya Shilingi milioni 6.
Baada ya upasuaji uliofanikiwa, alitoa shukrani zake kwa watu wote waliomtakia heri na waliomuunga mkono katika gharama za hospitali.
Social Plugin