Miili ya watu 27 wanaoaminika kuwa wahamiaji kutoka Ethiopia, "imetupwa" kando ya barabara katika eneo la Ngwerere kaskazini mwa mji mkuu wa Zambia, Lusaka.
Msemaji wa polisi nchini humo Danny Mwale amesema kwamba huenda waliuawa wakiwa katika usafiri.
Manusura mmoja aliyepatikana akipumua kwa shida amekimbizwa katika hospitali ya eneo hilo.
Zambia ni kituo cha usafiri kwa wahamiaji, hasa kutoka Pembe ya Afrika, ambao wanataka kuingia Afrika Kusini.
Bw Mwale alisema wakazi wa Ngwerere walipata miili hiyo leo Jumapili saa 06:00 mchana saa za eneo hilo .Alisema polisi wanaamini wahamiaji hao ni raia wa Ethiopia kulingana na stakabadhi za utambulisho zilizopatikana juu yao.
Miili hiyo imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Zambia.Katika nchi jirani ya Malawi, mamlaka iligundua miili 25 ya wahamiaji wa Ethiopia katika kaburi la pamoja mwezi Oktoba.
Social Plugin